Habari za Punde

Mvua za Vuli Zinazonyesha Zenj Tayari Baadhi ya Sehemu Zimeleta Madhara kwa Wananchi

Mwananchi wa maeneo ya Mtoni akipanga vipolo la mchanga kunusuru nyumba yake baada ya mvua zilizonyesha juzi kuleta madhara katika eneo la nyumba yake kupata mmomonyoko wa ardhi kutokana na kuzidiwa na maji ya mvua ilionyesha kwa muda wa karibu saa mbili. 

Baadhi ya nyumba katika eneo la mtoni Unguja ambazo zimejaa maji wakati wa kunyesha kwa mvua na kusababisha baadi ya nyumba hizo kuanguka kwa viambaza vyake kutoka na nguvu za maji hayo yaliokuwa yakipita kwa nguvu katika eneo hilo. na kujaa maji kwa muda.   
Moja ya nyumba iliopata madhara ya mvua za vuli katika maeneo ya mtoni Zanzibar ukiwa ukuta wake sehemu moja umeoanguka kutoka na mvua hiyo.

2 comments:

  1. Poleni wote mloharibikiwa InshaAllah M.Mungu akupeni subra amin. Lkn upande mwengine sisi wanaadamu huwa hatusikii, tukiambiwa tusijenge kiholela hatusikii, ona hizo nyumba zilivokaa hapo hata hayo maji hayana njia ya kupita

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau hapo Juu wazo lako tunaliheshimu lkn unaposema kujenga kiholela khasa una maana gani?? Kwani hapa Zanzibar wapi na wapi palipo jengwa kwa plan? Nitajie sehemu mbili tu. Shukuru Allah hapo ulipo pamesalimika na dhahma zozote. Kwa ujumla serikali imeshindwa kabisa kusimamia wananchi Juu ya Ujenzi bora ktk sehemu mwafaka zilizpimwa kiufundi na kuepusha majanga. Vikipimwa viwanja wsnsopewa ni hao hao, wazunguke, mskamishna wazima katibu mkuu, hakuna mnyonge wa mungu anathubutu kupata kiwanja kilichopimwa. Unafikiri watu wajenge wapi na vipi??

      Delete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.