Habari za Punde

Zanzibar Heroes hatarini kutolewa CECAFA yafungwa 4-0 dhidi ya Uganda Cranes




8

Wachezaji wa Uganda Cranes wakifurahia moja ya mabao waliyowafunga Zanzibar Heroes katika michuano ya CECAFA inayofanyika nchini Ethiopia

UGANDA imezinduka katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Zanzibar jioni ya leo mjini Addis Ababa, Ethiopia.


Huo unakuwa mchezo wa pili mfululizo kwa Zanzibar Heroes kufungwa, baada ya awali kugungwa 1-0 na Burundi na sasa inajiweka katika mazingira magumu kwenda Robo Fainali.

Mabao ya Uganda katika mchezo huo wa Kundi B yamefungwa na Farouk Miya dakika ya 10 na 18, Erisa Ssekisambu dakika ya 48 na Ceasar Okhuti dakika ya 79.


Zanzibar ilipoteza wachezaji wawili kwa kadi nyekundu katika mchezo huo, kwanza kipa wake Mwadini Ally dakika ya 13 na baadaye kiungo Mudathir Yahya dakika ya 74, wote wa Azam FC ya Dar es Salaam. Zanzibar itamaliza na Kenya wakati Uganda itamaliza na Burundi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.