Kampuni
ya simu za mikononi ya Halotel inaandaa matamasha ya Christmass katika mikoa
mitano nchini yenye lengo la kuwapa burudani watuamiaji wa mtandao huo pamoja
na wale watakaohitaji kujiunga na mtandao huo.
Matamasha
hayo ambayo yatafanyika wilaya za Tukuyu, Ruangwa, Moshi Vijijini, Chato pamoja
na Mpwapwa, yatajumuisha wasanii wa bongo fleva pamoja na burudani nyingine
kutoka kwa wasanii wa maeneo hayo.
Tamasha
la Halo Christmass wilayani Tukuyu litafanyika katika uwanja wa Tandale na
burudani itatolewa na wasanii Tundaman na Makomando.
Kwa
upande wa Ruangwa, tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya shule ya msingi
Likangala, na kutumbuizwa na wasanii Amini pamoja na Matonya, wakati Mpwapwa tamasha
litafanyika katika viwanja vya Mgambo likitumbuizwa na wasanii Madee na
Malaika.
Tamasha
hilo pia litafanyika wilayani Chato katika viwanja vya Stand ya Zamani huku
burudani ikitolewa na msanii Shetta na Baraka Da Prince.
Wakazi
wa Moshi vijijini pia watafurahia tamasha la Christmass kwa burudani Shilole na
Msami zitakazofanyika katika viwanja vya Kae.
Akizungumzia
matamasha hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Halotel bwana Nguyen Thanh Quang, amesema matamasha hayo ya Halotel
yanalenga kuwaleta watumiaji wa Halotel pamoja na kuwapa burudani ya kufunga
mwaka.
‘Hii ni zawadi kwa watumiaji wa mtandao wetu na wateja wapya wanaotaka
kujiunga na familia yetu ya Halotel, na ndio maana tunawafata katika maeneo yao
yalipo’ alisema Quang.
Matamasha hayo yatafanyika kuanzia saa sita mchana hadi saa kumi na mbili
jioni, na kiingilio itakuwa ni laini ya mtandao wa Halotel kwa wateja wapya
huku wale wenye laini za Halotel tayari wakiingia bure.
Quang pia amewaahidi wateja wa Halotel kuwa mtandao wake unatarajia
kuleta mabadiliko katika sekta ya mawasiliano nchini kwa kuwapa wateja wake
zaidi ya huduma za simu.
No comments:
Post a Comment