Habari za Punde

Kamati ya Olimpiki Tanzania Yafunga Mafunzo ya Walimu wa Michezo Skuli za Zanzibar.


Mkufunzi wa Mafunzo ya Walimu wa Michezo wa Skuli yaliyoandaliwa na   Kamati ya  Olimpiki Tanzania  (TOC) Suleiman Mahmoudu Jabiri  akitowa maelezo kwa washiriki  katika siku ya mwisho ya mafunzo hayo yaliyoanza  tarehe 01 mwenzi huu.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Mashavu  Faki akifunga mafunzo ya walimu wa michezo wa Skuli katika  Skuli ya Elimu Mbadala Rahaaleo Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Mashavu  Faki  akiwakabidhi vyeti washiriki  wa mafunzo  yaliyoandaliwa na Kamati ya  TOC  katika Ukumbi wa Elimu Mbadala Rahaleo Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Mashavu  Faki  akiwakabidhi vyeti washiriki  wa mafunzo  yaliyoandaliwa na Kamati ya  TOC  katika Ukumbi wa Elimu Mbadala Rahaleo Mjini Zanzibar.
Washirikiwa  mafunzo hayo wakiangalia kwa makini vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa na Mgeni Rasmin.Picha na Miza Othaman-Maelezo Zanzibar.

Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar.
Idara ya ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imeshauriwa kuwaandalia michezo nje ya nchi walimu wa michezo wa skuli kwa lengo la kujipatia taaluma zaidi na kukukuza mechezo nchini .

Hayo yameelezwa huko Rahaleo katika Ukumbi wa Elimu Mbadala na Watu wazima na Mkurugenzi Idaraya hiyo Zanzibar Mashavu Faki  wakati akifunga mafunzo yalioandaliwa na  Kamati ya Olimpiki Tanzania  (TOC) yaliyofunguliwa tarehe 1 mwezi huu.

Amesema iwapo walimu wa michezo watapatiwa mafunzo zaidi nje ya nchi wataweza kuwasomesha wanafunzi wao wa skuli na kuinua sekta  ya michezo Zanzibar.

Mkurugenzi Mashavu amesema katika mwaka 2013 kulifanywa utafiti wa kimchezo na kuonekana kuwa nchi zinazoimarisha michezo maskulini ndizo zinazofanya  vizuri zaidi katika masomo yao.

Aidha amesema michezo huimarisha afya, kujenga  upendo, udugu na uzalendo katika jamii hivyo hakuna budi kuendelezwa  kwa manufaa ya wanamichezo wenyewe na Taifa kwa jumla.

Sambmba na hayo Mkurugenzi huyo amewashauri waalimu waliopata mafunzo hayo kwa kushirikiana na Idara husika  kuandaa mafunzo kila baada ya miezi mitatu.

Nae mkufunzi wa mafunzo hayo Suleiman Mahamoud Jabir amewataka washiriki wa mafunzo hayo kujenga moyo wa kujitolea kwani katika kufundisha mara nyingi hujitokeza matatizo mengi.

Kwa upande wao waalimu waliopata mafuzo hayo Mussa Abdulrab na Arafa Talib Omar wamesema   wamejifunza mambo mengi wasioyajua na kuahidi kuwa watayafanyia kazi.

Mafunzo hayo ya siku tano ya walimu wa michezo wa skuli mbali mbali za  Zanzibar yameandaliwa na Kamati  Tanzania.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.