Habari za Punde

Naibu Waziri wa afya atembelea kituo cha afya Miwani

 Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Miwani, Wilaya ya Kati Unguja Fatma Keisi Ali akimtembeza Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo  sehemu mbali mbali za Kituo hicho kuona changamoto zinazowakabili ikiwemo tatizo la umeme, maji na upungufu wa wafanyakazi kituoni hapo.
 Kituo cha Afya cha  Miwani ambacho Naibu Waziri ameahidi kukiboresha ikiwa pamoja na kuondosha tatizo la umeme, maji na kujenga nyumba ya wafanyakazi. Picha Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
 Mmoja ya wananchi wa kijiji cha Miwani akimueleza Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (hayupo pichani) matatizo wanayoyapata kutokana na upungufu wa huduma muhimu katika kituo  hicho .

 Naibu Waziri wa Afya Mhmoud Thabit Kombo akiwasilikiza wananchi wa Miwani wakati alipofanya viara ya kutembelea kituo cha Afya cha Kijiji hicho kujua matatizo yanayokikabili kituo hicho,  (kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mohammed Saleh Jidawi.

 Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Miwani baada ya kusikiliza matatizo yanayokikabili kituo cha Afya cha Miwani.
 Daktari dhamana Kanda ya Unguja Dkt. Fadhil Mohd Abdalla akitoa ufafanunuzi baadhi ya masuala yaliyoulizwa na wananchi wa kijiji cha Miwani wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya katika kituo hicho.
Muuguzi wa Kituo cha Afya Miwani Fatma Keis Ali akielezea changamoto anazokabiliana nazo wakati wa kutoa huduma kituoni hapo ikiwemo upungufu wa wafanyakazi, tatizo la usafiri, maji na umeme.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.