Habari za Punde

Dk Shein Ajumuika na Waislam Katika Maadhimisho ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Viwanja vya Maisara Zanzibar.

Makamu wa Rais Mstaaf Dk Mohammed Gharib Bila akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maulidi ya Mfungo Sita Shilali alipowasili katika viwanja vya maisara kuhudhuria Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW,kitaifa yamefanyika katika viwanja vya maisara Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maulidi ya Mfungo Sita Sherali Champsi alipowasili katika viwanja vya maisara kuhudhuria hafla hiyo ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (A.S.W) Kitaifa yamefanyika Zanzibar katika viwanja vya Maisara. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Meya wa Zanzibar Khatib Abrahaman, alipowasili katika viwanja vya maisara kuhudhuria hafla hiyo ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (A.S.W) Kitaifa yamefanyika Zanzibar katika viwanja vya Maisara. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad alipowasili katika viwanja vya maisara kuhudhuria Maulidi ya Mfungo Sita Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad na Viongozi wa Dini na Serikali wakijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu Duniani kuadhimisha Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W yaliofanyika katika viwanja vya maisara Zanzibar. wakiwa wamesimami ikisomwa Qasida maalum ya ufunguzi wa hafla hiyo.
 Madressa Qadiria Tul Imaan ya Tomondo Zanzibar wakisoma Qassweeda maalum wakati wa hafla hiyo ya Maulidi ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.,A.W) katika viwanja vya Maisara Zanzibar.

Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sh.Khamis Haji Khamis akizungumza wakati wa hafla ya Maulidi ya Kuzaliwa Mtume (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya maisara Zanzibar.
Ustadh Juma Seif Said akisoma Quran Tukufu Surah Luwman wakati wa hafla hiyo ya Maulidi ya Kuzaliwa Mtume Muhammad yaliofanyika katika viwanja vya maisara Zanzibar.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sh. Khamis Haji Khamis akitia ubani kuashiria kuaza hafla ya kusomwa Maulidi ya Mfungo Sita yaliofanyika Kitaifa Zanzibar.katika viwanja vya Maisara.kulia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Naibu Mufti wa Zanzibar Sh. Mahmoud Mussa Wadi. 
Wanafunzi wa Madrasatul Nuhu Islamia ya Jangombe Zanzibar wakisoma Qasweeda ya Rabii Swahili. 
Ustadh Rashid Hamad Bakari akisoma Barzanji Mlango wa kwanza wakati wa hafla ya maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhammd (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya maisara Zanzibar.
Baadhi ya Wanafunzi wa Madrasa na Wananchi wa Zanzibar wakihudhuria hafla ya Maulid ya Mfungo Sita katika viwanja vya Maisara Zanzibar.
Ustadh Badru Mohammed Haji akisoma maulidi ya Barzanji Mlango wa Pili. 
Wanafunzi wa Madressa Ndandarawiya ya Bumbwini Mkoa wa Kaskazini A Unguja. wakisoma Qasweeda.
Ustadh Mzee Juma Mzee akisoma Maulidi ya Barzanji Mlango wa Tatu.
 Wananchi wakiwa katika viwanja maisara wakiitikia Maulidi ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Maisara Zanzibar.
Ustadh Abdul Rahaman Habshi, akisoma Qiyam Talaa pamoja na Madressa Al Nur Islamia ya Mkunazini Unguja Mji Mkongwe. 
Madressa Al Nur Islamia ya Mkunazini Unguja wakisoma Qasweeda ya Qiyam Talaa. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.