Habari za Punde

Balozi wa China Amtembelea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Lu Youqing , akisaini kitabu cha wageni mara baadaya kuwasili katika Ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia), ofisini kwake alipowasili Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ziara fupi.
 Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini, Lu Youqin akizungumza katika kikao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Charles Kitwanga (wa pili upande wa kushoto).  Katika kikao hicho kilichofanyika Wizara hapo, viongozi hawa walijadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Serikali ya China na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga (wa kwanza upande wa kulia), akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Lu Youqing (wapili upande wa kushoto) wakati wa mazungumzo yaliyohusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati Serikali ya China na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam..
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wa nne kutoka kulia), akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania, ulioongozwa na Balozi Lu Youqing (watatu kutoka kulia). Ujumbe huo ulitembelea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kujadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
(PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.