Habari za Punde

Kikundi cha Sarakasi cha Tunguu Kikisherehekea Mwaka Mmoja

Mgeni rasmi Simai Mohamed Said akizungumza na wana sarakasi baada ya maonyesho kwenye uwanja wa Kikungwi jana.Simai aliahidi kuwasaidia katika kuinua vipaji vyao kwa kuwatafutia nafasi za masomo ndani na nje ya nchi.
Mgeni rasmi Simai Mohamed Said akisalimiana na kijana Abdilah Abdalla (form one) kutoka kikundi cha Bihole cha kibele ambaye alikuwa kivutio kwenye maonyesho hayo.
Kikundi cha sarakasi kijulikanacho kwa jina la Nguva kutoka Kikungwi jimbo la Tunguu mkoa wa Kusini Unguja jana kilisherekea mwaka mmoja baada ya kusajiliwa rasmi ambapo katika sherehe hiyo Mgeni rasmi alikuwa mgombea uwakilishi wa jimbo la Tunguu, Simai Mohamed Said..
Sherehe hiyo ilijumuisha vikundi mbalimbali vya sarakazi kutoka mikoa mitatu ya Unguja ambayo ni, Nguva ktoka Kikungwi (wenyeji), Simba kutoka Mjimkongwe, Doldhin kutoka Nungwi, Kapoera kutoka Bububu, Bihole ktoka Kibele, New Star toka Mbarali na Fahari toka Magogoni.
Sherehe hiyo ilipambwa na wacheza muziki wa dansi kutoka kikundi cha Chokoleti kutoka Bungi mkoa wa Kusini Unguja
 Suleiman Aly kutoka kikundi cha Fahari cha Magogoni akionyesha umahiri wa mchezo wa Rolarola pamoja na kumbeba mchezaji mwenzake kichwani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.