Habari za Punde

DAWASCO Yabaini Wizi wa Maji Kiwanda cha Bahari Chemicals LTD

Moja ya kisima kinachodaiwa kutumika kuhifadhi maji yanayodaiwa kuibwa kutoka katika mtandao wa maji wa Dawasco.
Madumu ya Maji ambayo yame3kuwa yakitumika katka utengezaji wa maji ya Betri katika kiwanda cha Bahari Chemicals  Ltd.
Sehemu ya wizi wa maji kutoka katika mtandao wa DAWASCO unavyoonekana kufanywa katika kiwanda cha kutengenezea Betri cha Bahari Chemicals Ltd.

Ikiwa siku chache tu zimepita baada ya shirika la Majisafi 

na Majitaka Dar es salaam (Dawasco) kubaini wizi mkubwa wa Maji kutumika katika shamba la mboga mboga na matunda katika chuo cha Islamic kilichopo Boko ununio jijini Dar es salaam. Dawasco imebaini wizi mwingine wa Maji katika kiwanda cha kutengeneza Maji ya betri cha Bahari Chemicals Ltd kilichopo kurasini wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam.

Akizungumzia tukio hilo meneja wa Dawasco Temeke, Bw. 

Deogratius Rwegasira, amethibitisha kutokea kwa wizi huo 

ambapo kiwanda hicho kilikuwa kimejiunganishia Maji bila 

kibali cha Dawasco na kwamba hawakuwa na mita wala 

akaunti namba inayoonyesha kiasi cha Maji kinachopita 

katika system ya Maji iliyopo, na baada ya kufanya 

mawasiliano na Mkurugenzi wa kiwanda hicho 

Bw.Devendra Singh Parmar amekiri kutumia Maji hayo 

kinyume na taratibu .


“Baada ya kufanya uchunguzi tumebaini kuwa kiwanda hiki 

kimekuwa kikituibia Maji yetu kwa muda mrefu, mmiliki wa 

kiwanda amekubali kosa,lakini akisema kwamba wenyewe 

ni wageni hapa hawana zaidi ya mwaka mmoja tangu 

waanze kazi.hivyo hawakujua taratibu za kufuata”. Alisema 

Bw. Rwegasira.

Aidha meneja wa kiwanda hicho, Bw. Abdul Gulam, amekiri 

kuihujumu Dawasco kwa kuiibia Maji, lakini amesema kuwa 

wao ni wapangaji tu wamepanga katika eneo hilo na wana 

muda wa miezi saba tangu wahamie kiwandani hapo, 

walikuta wizi huo wa Maji ukifanyika katika kiwanda hicho 

na hawakujua taratibu husika za kufuata ili wapate huduma 

ya Maji kihalali.

“Sisi tumekubali kuwa tulikuwa tunatumia Maji ya 

DAWASCO bila kuyalipia, lakini sio sisi ambao 

tuliounganisha bomba hili, wapangaji waliopita 

walijiunganishia Maji haya hivyo tunaomba tulimalize hili, ili 

tuanze kuwa wateja wenu rasmi” alisema Bw.Gulam.

Aidha bwn Gulam ameainisha kuwa wao kama wamiliki wa 

kiwanda wamekubali kulipa faini iliyotolewa na DAWASCO 

ya Shiling million 3.5 ili warudishiwe huduma kama wateja 

wengine na waweze kuendelea na biashara.

Vitendo vya uhujumu wa Miundombinu ya Maji hususani 

wizi wa Maji unaendelea kuwa changamoto kwa 

DAWASCO licha ya kampeni na elimu inayotolewa kila siku 

juu ya uhalali na utaratibu wa kuungiwa huduma ya Maji 

inayotolewa na DAWASCO.

Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.