Habari za Punde

Uongozi wa Tasaf Pemba watembelea miradi

Sheha wa Shehia ya Mgelema, Omar Iddi Zaina , akitowa maelezo kwa wajumbe wa Kamati  ya Uongozi ya Tasaf  3 Pemba, juu ya Kitalu cha Mikarafuu  kilichoanzishwa na Walengwa wa Kaya maskini  katika Shehia hiyo.
 Mlengwa wa Kaya maskini katika Shehia ya Mlindo Wete, akihesabu fedha zake baada ya kupatiwa malipo kutoka kwa walipaji wa ruzuku ya Tasaf 3.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Tasaf Pemba, ambae pia ni mkuu wa Mkoa Kusini, akitowa maelezo kwa Wadau wa  mpango wa kunusuru Kaya maskini, katika Shehia ya Mlindo Wete.
 Mratibu wa Tasaf Pemba, Mussa Said Kisenge, akitowa maelezo juu malipo ya mpango wa kunusuru Kaya maskini kwa Wajumbe wa Kamati ya Uongozi huko Mlindo Wilaya ya Wete -Pemba.

Picha na Bakar Mussa-Pemba.

Katibu wa Kikundi cha Ushirika cha Mwanzo mgumu , Shemsa Ali Juma, kilichoanzishwa na Wadau wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini  katika Shehia ya Kinyikani , akitowa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya TASAF  Pemba,  juu ya walivyopiga hatuwa ya kuweka akiba kupitia fedha hizo na hatimae kuanzisha miradi kadhaa na kuitikia wito wa Tasaf kuweka kaiba na kuweza kuwasaidia pale tasaf itapomaliza muda wake.



Mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Tasaf Pemba, ambae pia mkuu wa Wilaya ya Chake Chake , Hanuna Ibrahim Massoud, akiangalia shuka lilifumwa na wadau wa mpango wa kunusuru Kaya maskini, huko Kinyikani Wete -Pemba.

Picha na Bakar Mussa -Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.