MRATIBU wa mafunzo ya kutambulisha kazi za
wasaidizi wa sheria Safia Saleh Sultan akielezea mafunzo hayo kwa waratib wa
shehia za Mkoa wa kaskazini Pemba, mafunzo yaliofanyika ukumbi wa mikutano wa
Kituo cha Huduma za Sheria Chakechake, kulia ni Mratibu wa Kituo Fatma Khamis Hemed
na katikati ni Afisa Mdhamini wizara ya wanawake na watoto Pemba, Mauwa Makame
Rajab, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WARATIBU wa shehia za mkoa wa kaskazini Pemba,
wakiwa makini kusikiliza mada zinazowasilishwa kwenye mafunzo ya kutambulisha
kazi za wasaidizi wa sheria, mafunzo hayo yameandaliwa na Kituo cha Huduma za
Sheria na kufanyika afisini kwao mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
AFISA Mdhamini wizara ya Uwezeshaji, Ustawi
wa Jamii Vijana Wanawake na watoto Pemba, Mauwa Makame Rajab akifungua mafunzo
ya siku moja ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, mafunzo yaliofanyika
Kituo cha Huduma za Sheria Chakechake, (Picha
na Haji Nassor, Pemba).
MTOA mada ya haki za binadamu Safia Saleh
Sultan kutoka Kituo cha Sheria, akiwasilisha mada hiyo kwenye mafunzo ya
kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, mafunzo yaliofanyika kituoni hapo
mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor,
Pemba).
MTOA mada ya dhana ya wasaidizi wa sheria
majimboni Fatma Khamis Hemed, kutoka Kituo cha Sheria, akiwasilisha mada hiyo
kwenye mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, mafunzo
yaliofanyika kituoni hapo mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment