Habari za Punde

ZLSC Yatowa Elimu ya Uraia Wanawake wa Vikundi vya Ushirika Pemba.

Afisa Mdhamini wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na watoto Pemba Mauwa Makame Rajab akifungua mafuno ya elimu ya uraia kwa wanavikundi wanawake wa Pemba, kulia ni mratibu wa mafunzo wa hayo Moahamed Hassan Ali na kushoto ni Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi Pemba Fatma Khamis Hemed, ambao ndio waandaji wa mafunzo hayo
Mratibu wa Mafunzo ya Elimu ya Uraia kwa wanawake wenye Vikundi vya Ushirika Ndg. Mohamed Hassan Ali kutoka kituo cha Sheria , akiwasilisha mada kwenye mafunzo yaliofanyika ZLSC Chakechake Pemba
Mtoa Mada juu ya haki za wanawake na changamoto zake,Bi. Fatma Khamis Hemed kutoka Kituo cha Sheria Pemba, kwenye mafunzo ya elimu ya uraia kwa wanawake wa vikundi mbali mbali kisiwani humo, mafunzo halifanyika kituoni hapo mjini Chakechake Pemba
Mkaguzi wa Uhamiji kutoka Mkoa wa kaskazini Pemba,Ndg. Omar Said Mohamed akiwasilisha mada juu ya uraia, kwa vikundi vya wanawake wa Pemba, mafunzo yaliofanyika Kituo cha Huduma za Sheria ZLSC tawi la Pemba
Afisa  Miapango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC Tawi la Pemba Ndg. Khalfan Amour Mohamed, akiwasilisha mada dhana ya utawala bora na demokrasia, kwa wanawake wenye vikundi vya ushirika, mafunzo hayo yaliandaliwa na ZLSC na kufanyika afisini kwao mjini Chakechake,
Wanawake wakiwa katika kazi za vikundi kwenye mafunzo ya elimu ya Uraia ilioandaliwa na Kituo cha Sheria Tawi la Pemba ZLSC, iliofanyika katika Ofisi ya Kituo hicho Chakechake Pemba. (Picha na Haji Nassor, Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.