Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais - Muungano na Mazingira, Mheshimiwa January Makamba akinyoosha mkono kuonesha
Mradi wa Kingo za Fukwe unaosimamiwa na
Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
wakati Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ilipotembelea Mradi huo jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya Waheshimiwa Wajumbe wa
Kamati ya Bunge ya Viwanda, Bihashara na Mazingira wakifatilia kwa makini
Taarifa ya Mradi wa Jengo la Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutoka kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza hilo, Mhandisi Bonaventure Baya (hayupo pichani).
Sehemu ya Waheshimiwa Wajumbe wa
Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakitembelea eneo la Mradi wa
Kingo za Fukwe jijini Dar es Salaam, mradi huo umeanzishwa kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi na unasimamiwa na Idara ya
Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Mheshimiwa January Makamba akiwa na Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakati wa walipotembelea Mradi wa Jengo la Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), anayetoa maelezo mbele yao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza hilo, Mhandisi Bonaventure Baya.
Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais
No comments:
Post a Comment