Habari za Punde

Mkoa wa Kusini Unguja Waingiza Timu Nne Sita Bora.

Na Mwandishi Wetu.

Mwishoni mwa mwezi huu wa Machi, mashabiki wa soka Zanzibar wanatarajiwa kushuhudia hatua ngumu ya sita bora kwa upande wa vilabu vya daraja la kwanza taifa Unguja.


Kikao cha pamoja kati ya kamati ya kuendesha mashindano chini ya mwenyekiti wake Mohammed Ali Tedy na viongozi wa vilabu hivyo leo umeapnga tarehe ya kuanza kwa hatua hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kamati hiyo kikao hicho kwa pamoja na ushirikiano wa uongozi wa Uwanja wa Amaan umekubaliana kuanza ngarambe hizo Machi 29.

"Tumeangalia majukumu ya kitaifa kama vile mechi ya kimataifa inayowakabili JKU, Uchaguzi mkuu wa Nchi na wiki ya Pasaka, tukaamua kwa pamoja tuanze ligi yetu mara baada ya kukamilika kwa shughuli hizo"

Mzunguko wa kwanza utakaoanza tarehe hiyo Chwaka itaivaa Strong Fire, White Bird itawafuata Taifa ya Jang'ombe huku Idumu ikimaliza mzunguko huo kwa kuvaana na Mundu.

Vilabu vya mkoa wa Kusini Unguja vilivyoingia hatua hiyo ni Chwaka, Strong Fire, White Bird pamoja na Idumu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.