Habari za Punde

Tutafika kweli?

Pichani tuiite foleni ya kupata tiketi za MV Mapinduzi 2 Chakechake, Pemba

Miaka ya zamani ilikuwa kila kitu kwa kibiru, ukitaka tiketi ya Sinema kibiru, tulipokuwa tukihangaika na mikate siku za shida ya miaka hiyo kibiru, pia kuliwa na wataalamu wa kibiru, ukiwapa tenda tu wanaingia kazini na kukupatia tiketi yako.

Utaratibu wa foleni ilikuwa ni msamiati usioeleweka.

Kinachoudhi hata ukileta ustaarabu wa foleni atatokea mtu eti anaingia moja kwa moja ndani na kudharau wote mlioko kwenye fulani kisa ana ujamaa na mhusika au na mfanyakazi wa hapo na wakati mwengine bila ya hata kuwaomba.

Tutafika kweli?


2 comments:

  1. Hilo ni tatizo sugu wakati mwengine ata kutia udhu msikitini unasubiri zamu yako basi anakuja mtu anakupiga kikumbo anaingia yeye

    ReplyDelete
  2. Kwa Zanzibar itachukua miaka elfu hadi tukakaa sawa

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.