Habari za Punde

Makamu wa Rais Mhe. Samia Afungua Kongamano la 21 kwa Watafiti wa Uchumi wa Viwanda.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti inayohusiana na maendeleo ya Ustawi Nchini (REPOA) Professa Yadon M Kohi, kabla ya kufungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda iliyoanza leo katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari  Beach jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti inayohusiana na maendeleo ya Ustawi Nchini (REPOA) Warsha hiyo imefunguliwa  leo katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari  Beach jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki, Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda baada ya kufungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa washiriki hao inayojadili kuhusu uendelezaji wa Utafiti wa Uchumi wa Viwanda Nchini. Warsha hiyo imefunguliwa leo katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari  Beach jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti inayohusiana na maendeleo ya Ustawi Nchini (REPOA) Professa Yadon M Kohi, baada ya kufungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda leo April 06,2016 katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es salaam. (Picha na OMR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.