Habari za Punde

Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Akutana na Uongozi wa Baraza la Tawla na Uongozi wa Skaut Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Baadhi ya Wawakilishi na Wanachama wa Chama cha SKAUT Nchini wakati ujumbe wa wawakilishi hao ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 27,2016 kwa ajili ya kumuelezea Makamu wa Rais shuhuli zao za kiutendaji hasa katika kutoa mafunzo mbalimbali kwa Mtoto wa kike.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na uongozi wa Baraza la Wanachama waChama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) wakati Uongozi huo ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 27,2016  kwa lengo la kumpongeza na pamoja na kumuelezea malengo na mikakati ya kiutendaji ya Chama hicho.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa SKAUT Nchini.

Makamu wa Rais Mhe. Samia akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Baraza la TAWLA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, na Katibu Mkuu Kiongozi Baolozi Peter Kijazi Baada ya kuapishwa Makatibu wa Mikoa April 27,2016 Ikulu Dar es salaam. (Picha na OMR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.