Habari za Punde

Balozi Mdogo wa Oman afariki Dunia Zanzibar

Aleyekuwa Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Balozi Ali Abdalla Al-Rashid aliyefariki Dunia juzi kwa usiku katika Hospitali ya Global kwa ugonjwa wa shindikizo la damu .
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wa serikali wakiuanga mwili wa Balozi mdogo wa Oman zanzibar bwa Ali Abdalla al-Rashid aliyefariki jana kwa ugonjwa shindikizo la damu katika hospital ya global zanzibar
 Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusafirisha mwili wa Balozi mdogo wa Oman nchini Zanzibar katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani karume Zanzibar


Na Mwandishi Wetu
Balozi mdogo wa Zanzibar aliyepo Zanzibar,  Mhe. Ali Abdallah Al-Rashid amefariki dunia  juzi usiku katika hospitali ya Global   baada ya kukabiliwa na shindikizo la damu.
Kufuatia kifo hicho,  viongozi mbalimbali wa vyama na serikali  na wananchi walishiriki kuuaga mwili wa marehemu  ambapo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliongoza  msiba huo.
Viongozi hao pia walishiriki   kuusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Oman kwa ajili ya mazishi katika Uwanja wa Ndege  wa Zanzibar kwa Shirika la Ndege la Oman  majira ya saa 8:00 mchana hapo jana.
Akizungumza kwa niaba ya  Serikali  ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif,  alisema Oman  na  Zanzibar zina uhusiano mkubwa katika kuimarisha mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja  na masuala ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni
.
Aidha, aliongeza kuwa  msiba huo ni  mkubwa siyo kwa Oman pekee lakini hata kwa Zanzibar  kwani umeacha pengo kubwa kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Balozi Seif pia alitoa pole  kwa wananchi wa Oman na Zanzibar kwa msiba huo.

Wakati huo huo, Mkurugenzi  Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Zanzibar, Balozi Silima Ali Kombo Haji, alielezea kusikitishwa na kifo cha Balozi Al-Rashid ambaye alikuwa  ni mtu mwenye hekima na busara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.