Habari za Punde

Balozi wa Kuwait Tanzania Afungua Madrasatul Qurania Kinuni Zanzibar Uliojengwa kwa Msaada na Kuwait.


Jengo la Madrasatul Quraania Kinuni Unguja limefunguliwa na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania likiwa na vymba vya madarasa vitatu kwa ajili ya watoto kusoma quran. 
Ustadh Hamad Khamis akisoma risala ya wananchi wa Kinuni wakati wa hafla ya uzindizi wa jengo hilo lililojengwa kwa msaada wa Kuwait
Mkurugenzi wa Africa Muslim Agency Zanzibar ,akitowa maelezo ya ujenzi wa Madrasa hiyo wakati wa ufunguzi wake uliofanyika huko Kinuni Unguja. 
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, akitowa nasaha zake kwa Wananchi wa Kinuni wakati wa uzinduzi wa madrasa yao iliojengwa kwa Msaada na Kuwait uzinduzi huo umefanyika huko kinuni Wilaya ya Magharibi A Unguja. 
Sheikh. Khamis Abdalla akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wananchi wa Kinuni katika sherehe za uzinduzi wa Madrasatul Quran Kinuni Unguja, Wilaya ya Magharibi A Unguja .

Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, akiwa katika hafla ya uzinduzi wa madrasa kinuni Zanzibar

Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, akimsikiliza mwanafunzi wa madrasa hiyo akisoma quran wakati wa uzinduzi wa madrasa yao huko kinuni unguja.
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, akimsikiliza mwanafunzi wa madrasa hiyo akisoma quran wakati wa uzinduzi wa madrasa yao huko kinuni unguja.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.