Habari za Punde

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Ziarani Mkoani Tanga.

Msafara wa Mapokezi ya Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alipowasili Mkoani Tanga kwa ziara ya Kikazi.
Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Mhe. Mustafa Mhina akimpokea Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg.Shaka Hamdu Shaka mara baada ya kuwasiri katika ofisi za CCM 

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka akipokelewa na Vijana wa Chipukizi na kumvisha Kiskafu ikiwa ishara ya kupokelewa katika Mkoa huo akiwa katika ziara yake ya Kikazi Mkoani Tanga.

Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka pamoja na Viongozi wa kitaifa alioambatana  wakisaini Vitabu vya wageni mara baada ya kuwasiri katika ofisi ya CCM Tanga
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tanga Ndg:Abdi Makange akimkaribisha Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shakakuzungumza na wanaCCM mkoani Tanga
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika Mkutano ulio fanyika katika ukumbi wa CCM mkoa lakini pia katika Mazungumzo yake alimtaka ,Mstahiki Meya kutopokea hongo za wapinzani ili kujiuzuru alisema ''MSTAHIKI MEYA TUNATAMBUA CHAMA CHA CUF KINATAKA KUKUPA HONGO ILI UJIZURU NAFASI HIYO NNAKUTAHADHARISHA KAMWE USIJARIBU KUKICHEZEA CHAMA CHA MAPINDUZI NA SISI KAMA VIJANA WA CCM TUNAKUTAKA KUPUUZA YOTE NA KUFANYA KAZI BILA VISHAWISHI VYOVYOTE ILI TUFIKIE MALENGO YA KUITEKELEZA ILANI YA CCM 2015-2020  UCHAGUZI UMEKWISHA SASA NI MUDA WA KAZI''

Mstahiki Meya Wa Jiji la Tanga Ndg.Mustafa Mhina akizungumza na kumhakikishia Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa ya kua kamwe hawezi kuyumbishwa na upinzani na Anawaahidi wana Tanga kufanya kazi kikamilifu ili kuleta maendeleo katika Jiji la Tanga.
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg.Shaka Hamdu Shakaakipokea wanachama Wapya toka Chuo Cha Utumishi Tanga

Wanachama Wapya Wakila kiapo cha Chama na Jumuiya zake.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.