Habari za Punde

Jumuiya ya Ismailia Charitable Trust Tanzania Yakabidhi Hundi Kuchangia Kambi ya Kipindupindu Zanzibar.

 Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Wizara ya Afya Zanzibar Dk Mohammed Dahoma akizungumza kabla ya hafla ya kukabidhiwa hundi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Ismailia Zanzibar Mr. Bhaloo, hafla hiyo imefanyika katika Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Ismailia Zanzibar Ndg Mohammed Bhaloo akizungumza wakati wa kukabidhi Cheki kusaidia Kambi ya Kipindupindu Zanzibar na kutowa shuikrani zake kwa Wizara ya Afya kwa ushirikiano wao na Taasisi mbalimbali zilizojitokeza kutowa misaada ya hali na mali na kuwataka Wananchi na Mashiriki kujitokeza kuchangia kambi hiyo ya Kipindupindu Zanzibar.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Ismailia Zanzibar Mr Mohammed Bhaloo akitowa maelezo kabla ya kukabidhi msaada wao kutoka kwa Familia ya Bhaloo na Jumuiya ya Ismailia Charitable Trust Tanzania kwa ajili ya kuchangia Kambi ya Kipindupindu Zanzibar. hafla hiyo imefanyika Wizara ya Afya Mnazi Mmoja.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Ismailia Zanzibar Mr Mohammed Bhaloo, akimkabidhi Hundi Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mohmoud Thabit Kombo iliotolewa na Ismailia Charitable Trust Tanzania. hafla hiyo imefanyika Wizara ya Afya Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi Hundi zilizotolewa na Jumuiya ya Ismailia Charitable Trust Tanzania na Familia ya Ndg Mohammed Bhaloo, Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dk Mohammed Dahoma, (Katikati) Mwenyekiti wa Ismailia Zanzibar Ndg Mohammed Bhaloo, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.