Habari za Punde

Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Wakabidhi Msaada kwa Kambi ya Kipindupindu Chumbuni.

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD) na Mwakilishi wa jimbo hilo Mhe Miraji Khamis Mussa wakiwa na viongozi wa Jimbo la Chumbuni wakitembelea kambi hiyo na kukabidhi misaada. 
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD) akisalimiana na Daktari Dhamana wa Kambi ya Kipindupindu Chumbuni Unguja Dk Ramadhani Mikidadi  

Daktari Dhamana wa Kambi ya Kipindupindu Chumbuni Unguja Dk Ramadhan Mikidadi akizungumzia hali ya maendeleo kwa Wananchi wanaolazwa katika kambi hiyo na kupata matibabu 

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD) katikati akizungumza wakati alipotembelea kambi ya kipindupindu chumbuni Zanzibar na kuwataka wananchi na Waheshimiwa kutowa misaada kwa wananchi wanaolazwa katika kambi hiyo na kumtaka Daktari dhamana kutowa taarifa ikiwa kuna baadhi ya vifaa kupungua katika kambi hiyo ili kuweza kupatika vifaa hivyo kupunguza kasi ya maambukizo ya mripoko wa maradhi ya matumbo.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD) akizungumza wakati wa kukabidhi msaada kwa ajili ya matumizi ya Wananchi waliolazwa katika Kambi ya Kipundupindu Chumbuni Unguja kulia Daktari Dhamana wa Kambi hiyo Dk. Ramadhani Mikidadi. 
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD)akimkabidhi boksi la biskuti Daktari Dhamana wa Kambi ya Kipindupindu Chumbuni Dk Ramadhani Mikidadi, hafla hiyo imefanyika katika Kambi hiyo Chumbuni Unguja. 
Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Mhe Miraji Khamis Mussa akimkabidhi boksi la biskuti Daktari Dhamana wa Kambi ya Kipindupindu Chumbuni Dk Ramadhani Mikidadi, hafla hiyo imefanyika katika Kambi hiyo Chumbuni Unguja. 
Daktari Dhamana wa Kambi ya Kipindupindu Chumbuni Dk Ramadhani Mikidadi akipokea msaada wa Katuni za Maji, Sabuni na Boksi za Biskuti kutoka kwa Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Mhe Ussi Salum Poindeza (AMJAD) wa tatu Mwakilishi Mhe Miraji Khamis Mussa.  
Daktari Dhamana wa Kambi ya Kipindupindu Chumbuni Dk Ramadhani Mikidadi akitowa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Chumbuni na Mwakilishi kwa msaada wao wa Katuni za Maji, Biskuti na Sabuni kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wanaolazwa katika Kambi hiyo, hafla hiyo imefanyika katika Kambi hiyo Chumbuni Unguja. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.