Habari za Punde

Timu ya Taifa ya Riadha Zanzibar U-20 Yapokelewa kwa Shangwe kwa Ushindi Walioupata katika Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati kwa Kuchukua Nafasi ya Nne ya Jumla


Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma akiwa na Viongozi wa Wizara hiyo wakisubiri kuwapokea Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Riadha ilioshiriki michuano ya Riadha ya Afrika Mashari U-20 Jijini Dar es Salaam wakiwa katikac Bandari ya forodhani Zanzibar. 

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Vijana U-20 akipeperusha Bendera ya Zanzibar akishuka katika boti ya Kilimanjaro wakirudi kushiriki michuano ya Riadha ya Afrika Mashariki yaliofanyika Jijini Dar es Salaam na kuibuka washindi wa Nne kwa Jumla.
Waziri wa Habari UItalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma akisalimiana na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Vijana wa U-20 wakati walipowasili katika bandari ya forodhani Zanzibar.
Waziri wa Habari Mhe Rashid Ali Juma akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana wa U-20 wakiwasili katika bandari ya Zanzibar 
Waziri wa Habari Mhe Rashid Ali Juma akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana wa U-20 wakiwasili katika bandari ya Zanzibar 
Wanamichezo wa Timu ya Taifa ya Riadha wakiwasili katika bandari ya Zanzibar na Boti ya Kampuni ya Azam Marine ya Kilimanjaro. wakitokea Jijini Dar es Salamaa walikoshiriki michuano ya Riadha ya Vijana wa U-20 kwa Nchi za Afrika Mashariki. 
Waziri wa Habari Mhe Rashid Ali Juma akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana wa U-20 wakiwasili katika bandari ya Zanzibar
Wachezaji wa Timu ya Vijana wa U-20 wakiwa katika bandari ya Zanzibar baada ya kuwasili na Boti ya Kilimanjaro V.
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma akisalimiana na Kiongozi alioongozana na Timu ya Taifa ya U-20 Khamis Gulam, wakati wa mapokezi ya Timu hiyo katika bandari ya Zanzibar. 
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Mwalim Khamis akizungumza wakati wa mapokezi ya Timu ya Taifa ya Riadha ya Vijana U-20, walipowasili katika Bandari ya Forodhani Zanzibar.
Wanamichezo wa Timu ya Taifa ya U-20 wakiwa katika ukumbi wa VIP wa Kampuni ya Boti za Azam Marine wakimsikiliza Waziri wa Habari akitowa nasaha zake na kuwapongeza kwa ushindi wao,
Rais wa Chama cha Riadha Zanzibar Ndg Abdulhakim Cosmas akizungumza wakati wa mapokezi ya Timu ya Taifa ya Vijana wa U-20 walioshiriki mashindano ya Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Chuom Kombo akiwapongeza Vijana wa Timu ya Taifa ya U-20 kwa ushindi wao katika mashindano ya Riadha ya U-20 kwa Vijana wa Nchi za Afrika Mashari yaliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhev Rashid Ali Juma, akimpongeza Kijana Ali Khamis Gulam kwa ushindi alioupatia Zanzibar kwa kushinda mbio za Mita Mia Moja na Mita Mia Mbili na kuweza kuvunja rikodi ya mbio hizo kwa mwaka huu kwa kukimbia Mita 100 kwa Sekunde.10;27 na kwa Mita 200 ameshinda kwa Sekunde 20;00 na kuimbuka mshindi wa mbio hizo na kuvunja redkodi hiyo na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Olimpiki kwa Vijana U-20. 
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma akizungumza na wanamichezo walioshiriki micchuano ya Riadha ya Vijana chini ya Umri wa miaka 20 yaliofanika Jijini Dar es Salaam na kuibuka washindi wa jumla kwa nafasi ya Nne kwa kujipatia Medali mbili ya Dhahabu kwa ushindi wa mbio za Mita Mia Moja na Mia Mbili kwa Wanaume.
Viongozi wa Timu ya Riadha walioongoza na Timu hiyo Jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo akitowa nasaha zake na kuwapongeza Vijana wa Timu hiyo ya U-20 kwa ushindi waliopata.

Wanariadha wa Timu ya Taifa ya U-20 wakiwa katika ukumbi wa VIP bandari ya Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Michezo Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma akiwapongeza kwa ushindi wao katika mashindano ya Riadha ya U-20 yaliofanyika Jijini  Dar es Salaam.   
Mshindi wa mbio za Mita 100 na 200 Ali Khamis Gulam akizungumza na waandishi wa habari za michezo Zanzibar jinsi alivyoonesha ari na ujasiri hadi kushinda katika mbio za mita mia na miambili na kuvunja rekodi ya mashindano hayo na kufuzu kushiriki michuani ya Olimpiki ya Vijana wa miaka U-20. kwa kuweka rikodi hiyo kwa mita miamoja amekimbia kwa sekinde 10.27 na kwa mita miambili amekimbia kwa Sekunde 20.00.na kunyakua Medali ya Dhahabu kwa kuwa mshindi wa kwanza wa mbio hizo.   
Mshiriki wa michuano ya Riadha  U-20 Tatu Sadun Makanjira akizungumza na waandishi wa habari kutokana na michuano hiyo ya Riadha U-20 jinsi ya mafanikio ya ushindi wao.katika kushiriki kwao katika michuano hiyo mikubwa kwa Nchi za Afrika Mashariki.
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Vijana U-20 Masoud Tawakal akizungumza na waandishi wa habari za michezo Zanzibar baada ya kuwasili Zanzibar wakitokea katika Michuano ya Kimataifa ya Riadha chini ya Vijana wa U-20. yaliofanyika katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. 
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa msafara wa Wanaridhaa wa Timu ya Taifa ya U-20, baada ya kuwasili katika bandari ya Zanzibar. 
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma, akiwa katika picha ya pamoja ya Wachezaji wa Timu ya Taifa wa Riadha ya Vijana wa U-20,baada ya kuwasili katika bandari ya Zanzibar wakitokea Jijini Dar es Salaam walikoshiriki michuano ya Kimataifa ya Riadha U-20 na kuibuka washindi wa Nne wa Jumla kwa kunyakua Medali mbili ya Dhahabu.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.