Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Atekeleza Ahadi Yake kwa Wananchi wa Jimbo lake.

Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Mifuko 100 ya Saruji Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Msingi ya Mahonda Bibi Kazija Moh’d Makame kutekeleza ahadi aliyopitoa wiki iliyopita ya kukibali kulifanyia matengenezo makubwa moja ya Jengo la Skuli hiyo lilikuko katika hali mbaya.
Balozi Seif akimkabidhi shilingi Milioni 5,000,000/- Fundi Mkuu wa matengenezo ya jengo la Skuli ya msingi Mahonda Bwana Haji Abdulla Omar hapo iliyopo skuli hiyo Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Balozi Seif akizungumza na Wanafunzi na Walimu wa Skuli ya Msingi Mahonda katika hafla ya kutekeleza ahadi aliyoitoa wiki moja iliyopita ya kugharamia matengenezo ya jengo la Skuli hiyo iliyoko katika mazingira hatarishi.
Kushoto ya Balozi Seif ni Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondri ya Mahonda Mwalimu Rashid Abdula, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pemba Juma na kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Mahonda Bwana Salum Gharib.
Mke wa Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mama Asha Suleiman Iddi akisisitiza umuhimu wa wananchi kuunga mkono juhudi za Wizara ya Elimu katika kuimarisha miundombinu ya ujenzi wa skuli mbali mbali Nchini.
Kushoto ya Mama Asha ni Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Mahonda Bwana Salum Gharib, Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif, Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mahonda Nd. Rashid Abdula, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pemba Juma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri.
Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma, wakipata maelezo kutoka kwa Fundi Mkuu wa Matengenezo ya Jengo la Skuli ya Msingi Mahonda wakati walipolikagua mara baada ya Balozi Seif kutekeleza ahadi yake skulini hapo.
(Picha na – OMPR – ZNZ.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.