Habari za Punde

Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Yasaidia Saruji kwa Ujenzi wa Vyoo vya Masjid Tasbih Kivunge Wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Meneja Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Mussa Mvita akizungumza na Uongozi wa Masjid Tasbih Kivunge Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya Masjidi hiyo, ili kuweza kutowa huduma kwa Waumini wa Kiislama wanapofika msikitini hapo, mwenye kazu Mshika Fedha wa Masjid Tasbih Sh. Ali Ama Ali na katikati Afisa Masoko wa PBZ Anas Rashid.hafla hiyo imefanyika katika masjid hiyo kivunge juzi. 
Meneja Masoko wa PBZ Ndg Mussa Mvita akisisitiza jambo wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi msaada wa saruji kwa ajili ya msikiti huo na hiyo ni sehemu ya mapato ya PBZ kutumia kwa shughuli za Jamii ambao ni wateja wa PBZ kunufaika na faida ya Benki yao.wakati wanapoweka fedha zao PBZ.
Meneja Masoko wa PBZ Ndg Mussa Mvita akikabidhi msaada wa saruji mifuko 50 kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa Vyoo vya Masjid Tasbih Kivunge Wilaya ya Kaskazini B Unguja, akipokea msaada huo Mshika Fedha wa Masjid Tasbih Kivunge Sh. Ali Ame Ali, makabidhiano hayo yamefanyika katika Masjid hayo huko Kivunge juzi.
Mshika Fedha wa Masjid Tasbih, Sh. Ali Ame Ali akishukuru Uongozi wa PBZ kwa msaada wao wa saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya Masjid yao tatizo hilo limekuwa ni moja ya kero kwa waumini wa msikiti huo kwa kukosa vyoo vya kutosha wakati wa Waumini wanapofika kwa ajili ya Ibada . Na kuwataka Wananchi na Waumini wac Dini ya Kiislam kuwataka kutowa michango yao kusaidia ujenzi huo. Na kusema wanahitaji matofali 1000, Mchanga Gari Mbili, Mabati 60, Miti ya Kuezekea na fedha ya Findi, kwa Mwananchi na Muumini wa Kidi ya Kiislam kuguswa na hali hiyo anaweza kuwasiliana na Uongozi wa Msikiti huo kwa kupitia Namba ya Simu 0772382346. ya Mshika Fedha Shekh. Ali Ame Ali.
Eneo ambolo linalotakiwa kujengwa kwa vyoo kwa ajili ya Masjid Tasnih Kivunge Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Mshika Fedha wa Masjid Tasbih Kivenge Sh. Ali Ama Ali akitowa maelezo kwa Maofisa wa PBZ walipofika kujionea hali halisi ya eneo hilo linalotaka kujengwa vya vyoo baada ya vyoo hivyo kubomolewa kutokana na kutokukidhi mahitaji ya Wananchi wanaofika katika Ibada msikitini hapo.
Mshika Fedha wa Masjid Tasbih Kivunge akimuonesha Meneja Masoko wa PBZ eneo ambalo linataka kujengwa vyoo katika msikiti huo. 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.