MENEJA Mkuu wa kampuni ya Evergreen Abdulghafar Ismail Mohammed akimfahamisha Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali juu ya hali ya chakula nchini alipotembelea katika ghala lake Saateni mjini Zanzibar.
BAADHI ya vyakula vilivyohifadhiwa katika ghala la kampuni ya Evergreen Saateni mjini Zanzibar.WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali akiwa katika maeneo ya kiwanda cha Zanzibar Miling Corporation Mtoni alipofanya ziara maalum kwa ajili ya kuangalia hali ya chakula nchini wakati huu wa kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhan.
WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali akioneshwa ngano na Meneja Mkuu wa kiwanda cha Zanzibar Milling kilichoko Mtoni Zanzibar Khalid Ali Yussuf, katika sehemu ya usagishaji alipotembelea kiwanda hicho.
MENEJA Mkuu wa kampuni ya Bopar Enterprises Said Nassir Said, akizungumza na Waziri Amina Salum Ali wakati Waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake Mombasa mjini Zanzibar.
PICHA ZOTE NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment