Habari za Punde

Kampuni ya Kanji Lalji Yatozwa Faini ya Shilingi Milioni Ishirini na Laki Tano

Naibu Waziri  Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupiga faini viwanda vitatu ambavyo vimetuhumiwa kuchafua mazingira wilaya ya temeke mtaa wa serengeti.                   
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh,Luhaga Mpina akipata maelezo kutoka kwa uongozi wa kiwanda cha bia serengeti alipofanya ziara ya kukagua Mazingira katika eneo hilo la viwanda linalotuhumiwa kuchafua mazingira. 
Naibu waziri  Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh, Luhaga Mpina akipata maelezo kutoka kwa mbunge wa temeke mh,Abdallah Mtolea kuhusu uchafuzi wa mazingira wilaya ya temeke mapema hii leo             

Na Evelyn Mkokoin. Dar es Salaam. 
Kampuni ya usafirishaji ya Kanji Lalji iliyopo mtaa wa Serengeti 

wilayani Temeke jijini Dar es Salaam imetozwa faini ya shilingi 

milioni ishirini na laki tano, na kutakiwa kulipa faini hiyo ndani ya 

siku saba, kwa kosa la kutiririsha maji yenye sumu katika mitaro 

ya maji ya mvua inayoelekea kwenye makazi ya watu na mazingira na hivyo kuhatarisha maisha na afya za viumbe hai.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira 

ametoa kauli hiyo leo kupitia Baraza la Taifa na Hifadhi ya 

Mazingira NEMC katika ziara yake ya kukagua viwanda na usafi 

wa mazingira jijini dar es salaam.


Ziara hiyo ya Naibu waziri Mpina, iliyopelekea naibu waziri huyo 

kuinuka Ofisini na kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika baadhi 

ya viwanda hivyo, imetokana na malalamiko ya baadhi ya wanachi katika maeneo husika hususan wenye viwanda.

Naibu waziri mpina amesema kuwa kutozwa faini ni hatua ya pili 

kwa baadhi ya viwanda baada ya kupewa onyo na maelekezo na 

NEMC na manispaa, na aliongeza kuwa kwa kutokutii taasisi za 

serikali baada ya adhabu hii hatua itakayofuata ni ya kuvifungia 

viwanda hivyo.

Kwa upande mwingine Mhe. Mpina amekipongeza kiwanda cha 

Serengeti breweries kwa kutii kauli ya serikali kwa kulipa faini 

iliyotozwa awali ya kiasi cha shilingi milioni kumi na sita kwa 

kosa la uchafuzi wa mazingira na kuwashukuru wakazi wanaozunguka kiwanda cha SBL pamoja na Mbunge wa TEMEME (CUF) Mhe.Abdallah Mtolea kwa kutoa taarifa za uchafuzi wa mazingira na kukipa kiwanda hicho siku 45 kufanya marekebisho madogo madogo ya kimazingira kiwandani hapo.


Aidha, Adhabu nyingine ya uharibifu na uchafuzi wa mazingira 

imetolewa kwa wamiliki wa eneo la kampuni ya CI group, ambao 

ni Prime Liberty Limited ya kutakiwa kulipa faini ya shilingi 

milioni 15 kwa muda wa siku saba, na kufanya jumla ya faini za 

uchafuzi wa mazingira zilizotozwa kwa siku ya leo kuwa shilingi 

milioni 39 na laki tano.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.