Habari za Punde

Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Kikwete Afungua Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Ukumbi wa Dodom Convention Center

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Mhe,Abdulrahman Kinana (katikati) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(kushoto) akifuatiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ,Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMzee Ali Hassan Mwinyi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Bara mhe,Philip Mangula(kulia) wakisimama kuimba wimbo wa  Taifa kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM wa Kumchagua mwenyekiti mpya wa tano wa chama hicho uliofanyika leo Mjini Dodoma


Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahman Kinana akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais Mstaaf Mwenyekiti wa CCM Taifa kuufungua Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Mjini Dodoma leo. 
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete(katikati) akitoa hutuba yake wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM wa Kumchagua mwenyekiti mpya wa tano wa chama hicho uliofanyika leo Mjini Dodoma (kushoto)Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Makamo mwenyekiti wa CCM Bara mhe,Philip Mangula 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.