Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein, Afanya Uteuzi wa Wakurugenzi na Manaibu Katibu.

Taarifa kwa Vyombo vya Habari Uteuzi wa Wakurugenzi na 

Manaibu Katibu 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbali mbali za serikali.

Wateule hao ni Dk. Juma Yakout Juma kuwa naibu Katibu Msaidizi wa Baraza la Mapinduzi na Mwadini Makame Haji kuwa Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala bora, walioteuliwa ni Abdulla Issa Mgongo kuwa Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti na Shaibu Ally Mwazema kuwa Mkurugenzi wa Miundombinu ya Taasisi, Utumishi na Maslahi ya watumishi.

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ,
Khalid Omar Abdulla anakuwa Mkurugenzi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakati Mashaka Hassan Mwita ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Magharibi A.

Katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,  Issa mlingoti Ally anakuwa Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ Dar es salaam, Ameir Makame Ussi, Mkurugenzi Idara ya Mipango, Sera na Utafiti na Khalid Bakari Amran, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali.

Wengine ni Riziki Daniel Yussuf aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Idara ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa huku Ali Salim Matta akipewa nafasi ya Ofisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba.
Wizara ya Afya walioteuliwa ni Ramadhan Khamis Juma kuwa Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti na Ofisa Mdhamini Pemba ni Ali Bakari Ali.

Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Haji Hamid Saleh anakuwa Mkurugenzi Umwagiliaji Maji.Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo, ni Dk. Omar Abdulla Adam anakuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni.


Katika  Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, walioteuliwa ni Abdulla Mwinyigogo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba na Ramadhan Mussa Bakari kuwa Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo, ambapo  Omar Ali Omar Bhai anakuwa  Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi katika
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira, walioteuliwa ni Tahir M. K. Abdulla kuwa Naibu Katibu Mkuu, na Hemed Salim Hemed anakuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Huduma za Maji na Nishati (ZURA).

Nana Mwanjisi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko.

Imetolewa na idara ya habari maelezo-zanzibar

Julai 20,  2016

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.