Habari za Punde

Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) kwa Kushirikiana na Kampuni ya Simu ya Zantel Wamerudisha Huduma ya Ezypesa kwa Wanunuzi wa Umeme kwa Njia ya Simu.


Mkurugenzi mkuu wa Zantel nchini, Benoit Janin (kulia) akiongeza kwenye mkutano na wandishi wa habari jana kwenye ofisi za shirika la Umeme, Gulioni mjini Zanzibar jana.Kushoto ni Mkurugenzi wa shirika la umeme Zanzibar, Hassan Ali Mbarouk.

Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Zanzibar, Hassan Ali Mbarouk (kushoto) akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu kurejeshwa kwa huduma ya kununua umeme kwanjia ya simu Ezypesa jana.
Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa Zantel nchini, Benoit Janin

Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakifuatilia mkutano huo wa kutowa taarifa ya kurudisha huduma ya kununua umeme kupitia Ezypesa huduma hiyo inayotolewa na Kampuni ya Zantel mkutano huo umefanyika Shirika la Umeme Gulioni Zanzibar.(Picha na Martin Kabemba)

Zanzibar, 21 Juni-2016: 
Kampuni ya simu ya ZANTEL kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Zanzibar, ZECO, leo wamezindua upya huduma ya kununua umeme kwa kutumia huduma ya Ezypesa visiwani Zanzibar.

Huduma hiyo inayojulikana kama TUKUZA, ilisitishwa miezi michache iliyopita kutokana na hitilafu za kiufundi, na sasa imeboreshwa zaidi kuweza kuhudumia wateja wengi zaidi na kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa huduma hiyo, Afsa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Bw. Benoit Janin, alisema Zantel itaendelea kuwa msitari wa mbele kutoa huduma zitakazorahisisha maisha ya wateja wake.

'Toka kampuni ya Millicom ilipoingia, tuliahidi kuboresha huduma zetu, lakini pia kuhakiskisha huduma hii ya TUKUZA inaanza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa, na leo tuna furaha kuizindua huduma hii tena, na kwa uwekezaji tuliofanya tunaamini hakutakuwepo na hitilafu tena’ alisema Janin.

Maboresho hayo katika huduma ya TUKUZA yanatarajia kuwapa faida mbalimbali wateja wa ZECO na Zantel ikiwemo kuongezeka kwa spidi ya mfumo, pamoja na kumaliza kabisa tatizo la foleni katika vituo vya ZECO.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ZECO, Bw Hassan Ali Mbarouk, alisema kuboreshwa kwa huduma hiyo ni hatua muhimu ya kuwawezesha wateja wa visiwani humu kupata huduma bora na pia kuongeza kipato kwa mawakala wa Ezypesa.

'Kupitia simu zao za mikononi wateja wetu wataweza kutumia huduma ya Ezypesa kununua umeme  na kulipia bili zao, mahali popote na kwa muda wowote na hivyo basi kupunguza gharama za kwenda kwenye vituo vya ZECO kununua umeme’ alisema Mbarouk.


Huduma ya Ezypesa, pamoja na kutoa huduma ya TUKUZA pia inatoa fursa mbalimbali kama kuweza kuhamisha fedha kwenda mitandao mbalimbali pamoja na kufanya miamala kupitia benki ya Watu wa Zanzibar, huku pia ikiwa katika mpango wa kuhalalishwa na Mufti wa Zanzibar.

1 comment:

  1. Kuhalalishwa na mufti mkuu ndo vipi hapo ? Naona kama haijakamilika hio habari ya Mufti. Kwa nini serikali isilipe mshapata Kwa katumia hio huduma ili kuondokana / kupunguza mishahara hewa?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.