Habari za Punde

Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Jakaya Kikwete Afungua Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM Mjini Dodoma leo.

Rais Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya White House akihudhuria Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM, akiwapungia mikono Wananchi na Wanachama wa CCM waliofika katika viwanja hivyo leo asubuhi. 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahaman Kinana wakielekea katika ukumbi wa Mkutano katika jengo la White House Dodoma leo asubuhi.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli wakati akiwasili katika viwanja vya Afisi ya CCM White House Dodoma kuhudhuria Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM iliokaa leo asubuhi. 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahaman Kinana, kushoto Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli. 
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahaman Kinana wakielekea ukumbi wa mkutano baada ya kuwasili katika viwanja vya Jengo la Ofisi ya CCM Mjini Dodoma White House.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli wakifurahia jambo wakati wakielekea ukumbi wa Mkutano white house Mjini Dodoma leo asubuhi.
Wajumbe wa Mkutano wa Kamati Kuu wakiwa katika ukumbi wa Mkutano wakibadilishana mawazo kabla ya kuaza kwa mkutano huo 
Wajumbe wa Mkutano wa Kamati Kuu wakibadilisha mawazo kabla ya kuaza kwa Mkutano wa Kamati Kuu Mjini Dodoma leo asubuhi.
 Wajumbe wa Kamati Kuu wakiwa katika ukumbi wa mkutano kulia Dk Salim Ahmeid Salim na Mhe Hussein Mwinyi wakibadilishana mawazo kabla ya kuaza kwa mkutano huo.
Wajumbe wa Mkutano mkutano wa Kamati Kuu ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa. 
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiwa katika ukumbi wa mkutano White House kutoka kulia Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid, Mhe Sadifa Mhe Shamsi Vuai na Mhe Ali Salum. wakisubiri ufunguzi wa mkutano huo.  
Viongozi wa meza Kuu wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Jakaya Mrisho Kikwete katikati na kulia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na kushoto Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahaman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndg Philip Mangula wakisimama baada ya kuingia katika ukumbi wa mkutano wa Kamati Kuu ya CCM Mjini Dodoma leo 

Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahaman Kinana akitowa maelezo kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Jakaya Mrisho Kikwete kufungua mkutano huo wa Kamati kuu kujadili jina la Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa. mkutano huo umefanyika katika Ofisi za CCM White House Dodoma 
Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo, katika ukumbi wa Ofisi za CCM White House .  
 Wajumbe wa Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.