Na:
Mwandishi Wetu.
Mkuu
wa Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Shaibu Issa Ndemanga, leo ametembelea katika
Shule ya Sekondari ya Lindi iliyopo katika manispaa ya lindi mjini kwa lengo la
kuanza ujenzi wa shule hiyo ikiwa ni agizo la Waziri mkuu Kassimu Majaliwa
ambaye aliitembelea shule hiyo ivi karibuni baada ya kuungua Moto na kuteketeza
zaidi ya madarasa 8 katika shule hiyo.
Mkuu
huyo wa Wilaya ambaye ameanza utendaji wake kwa kasi ikiendana na Kasi ya
serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa jamhuri ya Muungano John Pombe
Magufuli, aliitembelea shule hiyo kwa lengo la kuangalia changamoto zilizopo
ikiwa ni pamoja na kujadili suala la Ujenzi wa barabara itakayotumika kwa ajili
ya kuhakikisha vifaa vya ujenzi wa shule vinafika kwa usalama katika eneo hilo
la madarasa wakati huu ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza mara moja.
Akizungumzia
ujenzi wa shule hiyo Mkuu huyo wa Wilaya
ya Lindi Mjini alisema kuwa analazimika
kufuatilia suala hilo lifanyike kwa haraka kutokana na kuwa agizo lililotolewa
na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa alipotembelea shule hiyo wakati wa uchangiaji
wa harambee kwa alengo la kufanikisha ujenzi huo kupitia wadau mbalimbali
waliochangia Ujenzi wa Shule hiyo.
“Siyo
jambo la taratibu hili, maana ni maagizo ambayo yametolewa na Mheshimiwa Waziri
Mkuu kwamba ufanyike kwa haraka iwezekanavyo, kwa hiyo mimi nafuatilia kutimiza
Kauli ya Waziri Mkuu ambaye alisimamia uhamasishwaji wa uchangiaji wa ujenzi wa
majengo ya Shule yalioungua kwa Moto, na kama unavyoona mwenyewe tayari wadau
wameendelea na zoezi la kutoa kile walichosema watatoa, na hapa leo nakagua
kwanza Sehemu ya Barabara ambayo itajengwa kwa dharura ili kufikisha Vifaa eneo
la Ujenzi lakini si hivyo tu hapa kuna changamoto nyingi ambazo zinatakiwa
kufanyiwa ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kupata mchoro wa jingo ambao unatakiwa
uandaliwe kwa haraka na siyo vinginevyo, pili ni kwa hawa wajenzi ambao
wanatakiwa kubuni barabara mbadala ambayo pamoja na kwamba itatumika kwa ujenzi
huu lakini pia iwe ni barabara ambayo itakuwa ya kudumu kwa lengo la kuja
kusaidia wakati mwingine kama itatokea tatizo kama hili, kitu kingine ni jinsi
ambavyo wajenzi wanatakiwa kubuni mchoro wenye kiwango kwa ajli ya kuendana na dunia
ya sasa, siyo tu bora mchoro, wahakikishe mchoro huo unakuwa kivutio na jingo
lenyewe liwe ni jingo linalokidhi mahitaji kwa ajili ya shule hii, pamoja na
kwamba changamoto ni nyingi lakini pia nimefika hapa kuangalia kile ambacho
tayari kimepatikana na wapi kimehifadhiwa, si unajua unaweza kupata lakini
ukose sehemu ya kuhifadhi, tunatarajia kupokea mifuko ya Simenti kutoka Dangote
zaidi ya 4000 na mabati kama 400 ivi kwa hiyo ni lazima nifahamu ni wapi
itakuwa stoo ya kuifadhi hivyo vifaa, na nataka kusimamia mimi mwenyewe ujenzi
huu kwa haraka ili kutimiza maagizo ya Waziri Mkuu “ alisema Ndemanga
Na kuongeza kwamba ujenzi huo tayari umeanza
rasmi na hivyo zoezi la kwanza ni kuangalia jinsi ambavyo utaratibu wa kubomoa majengo yaliyoungua na
uzoaji wa vifusi utakavyofanyika na wakandarasi bila kuathili shuguli za
kimasomo za wanafunzi wanaoendelea na shuguli zao za kimasomo hapa shuleni.
Katika
Ziara hiyo ya ukaguzi wa maeneo ya ujenzi Mkuu wa Wilaya alifuatana na
Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Mjini
Bwana Jomaary Mrisho Satura,
pamoja na Mkandarasi wa Majengo aliyekabidhiwa ujenzi huo wa majengo ya shule hiyo ya Lindi Sekondari Engeneer Lusekelo Mwakyami ambao kwa
pamoja waliweza kushirikiana kimawazo
kushauriana na Mkuu huyo wa Wilaya kuangalia maeneo ambayo kunatakiwa Barabara
ipite, ikiwa ni pamoja na kushauliana kuhusu Nguzo za tanesco zilizopo maeneo
hayo ya ujenzi wa Majengo ya Shule, Mitaro iliyopo kwa ajili ya kupitisha maji
wakati mvua zinaponyesha , pamoja na kuangalia maeneo ya viwanja vya michezo
ili yasijekuharibiwa na ujenzi huo.
Aidha
waliweza kushauriana pia namna ambavyo kwenye ujenzi huo ambayo utakuwa wa
ghorofa na siyo ujenzi wa madarasa ya chini, kuangalia jinsi ambavyo wachoraji
wa ramani wanatakiwa kuweka njia za magari ambayo yatapita hadi eneo la wazi au
kuweka parking za magari ya viongozi na siyo tu kuishia mbali kama ilivyokuwa
hapo awali.
“tunafikilia
kuwa jingo hili ambalo ni ghorofa liwe na maeneo ya parking za magari, yaani
magari yawekewe njia za kupita, naamini kwamba
katika majengo haya kutakuwa na idadi kubwa za maofisi ya walimu pamoja
na kwamba kutakuwa na madarasa pia, hivyo walimu ambayo watakuwa na vyombo vyao
vya usafiri au magari ya serikali yaweze kuingia hadi maeneo haya ya Majengo
kwa ndani, maana majengo haya tunatarajia kwamba yatakuwa ya kisasa nay a
kupendeza na yatakayokuwa yameendana na duania ya sasa, na ndiyo maana umetuona
sisi wote, Kaimu mkuu wa Mkoa, ambaye ni DC wetu, mkandarasi wa Manispaa na
mimi Mkurugenzi wote tumefika ili kujadiliana kwa umakini suala hili ili baada
ya ujenzi kusipo na maswali kutoka kwa wakuu wetu” alisema Satura
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya mheshimiwa Shaibu
Ndemanga, alisema kuwa yeye mwenyewe atakuwa ni mionmgoni mwa wajenzi wa
majengo kutokana na kwamba ni wajibu wake kuhakikisha kila siku anawasili
kukagua hatua kwa hatua hadi ujenzi utakapokuwa umekamilika.
Ivi
karibuni Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa wakati wa Ziara yake mkoani lindi alitoa
agizo la kuharakishwa ujenzi wa shule hiyo huku yeye mwenyewe akiwa ni miongoni
mwa viongozi waliofika wakati wa uchangiaji wa harambee ya kuhakikisha kiasi
cha fedha kinapatikana kutoka kwa wadau mbali mbali wa Elimu wa mkoa wa lindi
kwa lengo la kufanyika kwa ujenzi wa shule hiyo.
No comments:
Post a Comment