Habari za Punde

Serikali Yaanzisha Mpango Maalum wa Upimaji wa Ardhi na Urasimishaji wa Maeneo Yasiopimwa Jijini Dar es Salaam

Meneja wa kituo cha huduma kwa Wateja Bw.Juma Msabaha akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja kilichozinduliwa hii leo Makao makuu ya Benki hiyo,Golden Jubilee towers Daresalam. Sasa wateja na wasiokuwa wateja wa benki hiyo wataweza kupata maelezo kuhusiana na mikataba ya mikopo inayofuata mifumo ya kiislamu, kutoa msaada katika matumizi ya huduma zetu mbadala kama ATM, Internet Banking, Amana Bank Mtaani, Amana Mobile na huduma nyingine mbalimbali.

Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria Mkutano huo wakisikiliza kwa makini uzinduzi wa kituo hicho. Imeelezwa kuwa kituo hicho kitasaidia kusogeza huduma karibu na wananchi na kutatua baadhi ya kero ambazo wateja walikuwa wanakutana nazo.

Mkuu wa biashara wa AMANA BENKI  Bw. Munir Rajab akifafanua jambo  kuhusu kituo hicho.

NA SELEMANI MAGALI- DARESLAAMBENKI ya Kiislamu ya Amana imezindua kituo chake kipya cha  huduma kwa wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu ikiwa ni sehemu ya mkakati wao wa kuboresha huduma kupitia teknolojia ya mawasiliano
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam,Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja  wa Benki hiyo Bw. Juma Msabaha alisema uzinduzi wa kituo hicho umelenga kuboresha mahusiano ya wateja pamoja na kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi.

Akifafanua kuhusu kituo hicho, Bw. Msabaha alisema kituo hicho kitafanya kazi kwa masaa 15 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nne usiku ambapo wateja wa Amana na ambao bado hajabahatika kutumia huduma za benki hiyo watapata fursa ya kuuliza masuala mbalimbali kuhusu huduma zinazotolewa na Benki.
“Tumejipanga vizuri, tunayo timu nzuri yenye uzoefu na masuala ya Kibenki ,watafafanua mambo mbalimbali kuhusu huduma za Amana benki kuanzia masuala ya akaunti,miamala ya kimtandao na huduma zinazotolewa na mawakala wetu kote nchini.Alisema Msabaha.
Ameongeza kusema Kituo hicho kitafanya kazi  siku saba katika wiki,pamoja na siku za siku kuu jambo ambalo wanaamini litasaidia kufafanua mambo mbalimbali yanayowahusu wateja.
“Namba yetu ya huduma kwa mteja ni 0657 980 000, kupitia namba hiyo ni matarajio yetu kuwa wateja watafurahia zaidi huduma tuliyoizindua kwani ni rafiki kwa kila mmoja, imeandaliwa mahususi kabisa kuwapa uwezo wananchi kupiga simu,kutuma ujumbe mfupi pamoja na njia zingine za mitandao ya kijamii”.Alisema Msabaha
Kwa mujibu wa Bw Msabaha kituo hicho kinatarajiwa kuleta mabadiliko kwenye biashara
kupitia huduma za kibenki huku akiongeza: “Ni adhma yetu kuhakikisha kwamba tunapambana siku zote ili tu hali ya kiuchumi kwa wateja wetu iendelee kuwa bora na ni  hicho tu ndio kimekuwa kikitusaidia kuwa na matokeo mazuri
Alibainisha kuwa huduma hiyo ilibuniwa mahususi ili kuleta tija kwa wateja wa benki hiyo kwa kuwa inaenda sambamba na mahitaji yao, mfumo wao wa maisha pamoja na hadhi yao hatua aliyoilezea kuwa itaiongezea benki hiyo uaminifu miongoni mwa wateja wake
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Biashara ya Amana Benki Bw. Rajab Munir amesema wateja wa Amana watapata fursa ya kuijua benki yao kwa undani kwani sasa wanaweza kuulizwa maswali yao na kujibiwa kwa wakati ndani ya masaa 15 katika wiki ikiwamo siku za siku kuu.
Alisema hiyo ilikuwa dhamira yao ya muda mrefu na kuzinduliwa kwake imekuwa ni faraja kwa wateja ambao sasa watafaidika nayo.kwa kupata majibu ya papo kwa hapo kuhusiana na akaunti zao, miamala yao na misaada kuhusu kutumia huduma za kimtandao.

katika kipindi kisichopungua miaka mitano Tayari Benki ya  Amana kwa  imefanikiwa kuwa na matawi saba matano yakiwa katika Jiji la Daresalaam na mengine mawili yakiwa katika Jiji la Mwanza na Arusha.
Mipango ya Baadae ni kwamba Amana benki inatarajia kufungua matawi mengine  si chini ya matatu kati ya Mkoa wa Tanga au Zanzibara kulingana na upembuzi yakinifu utakaofanywa  na benki hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.