Habari za Punde

Ziara ya Mbunge na Mwakilishi Jimbo la Kikwajuni Kutembelea Miradi Barabara na Uwekaji wa Taa.

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Mwakilishi wakitembelea ujenzi wa barabara hiyo kujionea maendeleo yake inayojengwa na kampuni ya Mecco Tanzania.

Wafanyakazi wa Kampun i ya Ujenzi wa barabara ya Mecco wakiweka tuta katika barabara hiyo ili kuepusha ajali kwa watumiaji wa barabara hiyo kupunguza mwendo kasi wa vyombo vya moto.
Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Nassor Salum Jazira akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yao kutembelea miradi ilioko katika jimbo hilo.akiwa na Mbunge na Madiwani wa jimbo hilo. 
Barabara ya Kikwajuni ikiwa katika kiwango baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa wa kuwekwa lami mpya kuanzia klabu ya Kikwajuni hadi Maisara, 
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar, Mhe Eng Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwa katika ziara yake kutembelea ujenzi wa barabara katika jimbo lake katika kiwango cha lami.
Sagamawe la kampuni ya Mecco inayojenga barabara ya Kikwajuni likiweka sawa lami katika barabara hiyo na kuweka tuta kwa ajili ya kupunguza mwendo kasi wa watumiaji wa vyombo vya moto kuepusha ajali kwa watembea kwa miguu.
Mwakilisho wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Nassor Salum Jazira akizungumza na Mainjinia wa kampuni hiyo wakati wa ziara yao kutembelea mradi huo kuona maendeleo yake katika jimbo lao. 
Eng wa Kampuni ya Central Electricals akitowa maelezo kwa Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni wakati wa ziara yao kutembelea mradi huo unavyoendelea katika jimbo hilo ukiwa katika hatua za mwisho za ukamilikaji wake na kutowa huduma kwa wananchi wa jimbo hilo wakati wa usiku. 
Mafundi wakiwajibika kuweka waya wa taa hizo.
Mafundi wa kampuni ya Central Elecrticals wakiweka waka katika moja ya nguzo za taa hizo zinazotumia nguvu ya jua (solar) katika moja ya barabara za jimbo la Kikwajuni Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng. Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake kutembelea Miradi ilioko katika Jimbo la Kikwajuni ya uwekaji wa Taa za Solar na uwekaji wa lami katika barabara ya kikwajuni kutokea klabu ya kikwajuni hani maisara. akiwa na  Maijinia wa Kampuni ya Uwekaji wa Taa hizo kutoka Kampuni ya Central Electricals Tanzania. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.