Habari za Punde

Ziara ya Waziri wa Kilimo wa Tanzania na wa Zanzibar Kutembelea Bonde la Mpunga la Cheju Wilaya ya Kati Unguja.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Zanzibar akizungumza wakati wa Ziara ya Mawaziri wa Kilimo wa Zanzibar na Tanzania Bara katika bonde la Mpunga la Cheju kujionea hasara waliopata wakilima wa bonde hilo kwa kukosa mpunga wao kutokana na mvua za masika kukata hafla na kusababisha hasara hiyo.
Waziri wa Kilimo Mifugo Uvuvi Tanzania Bara Mhe Dk. Charles John Tibeza aliyeshika mikono akimsikiliza Mkulima wa Mpunga wa Bonde la Cheju Wilaya ya Kati Unguja Ndg.Omar Iddi Golo,akitowa maelezo ya hasara waliopata kutokana na mashamba yao ya mpunga kukosa maji kutokana na mvua za masika kunyesha kwa muda mfupi na kukata kunyesha. mwenye miwani na kofia Waziri wa Kilimo Mifugo Uvuvi na Maliasili Mhe Hamad Rashid Mohammed.
Mkulima wa Mpunga Bonge la Cheju akionesha mashamba ya mpunga yalioharibika kwa kukosa mvua wakati wa msima wa kilimo hicho katika bonge hilo.
Mkurugenzi Idara ya Kilimo Ndg Mohammed Khamis Rashid, akitowa maelezo kwa Mawaziri hao wakati walipofika katika bonde hilo kujionea hasara hiyo iliowapata wakulima wa mpunga wa bonge hilo.kwa kukosa mavuno kwa msimu huu kutokana na mpunga wao kuharibika kwa kukosa maji ya mvua. Mashamba ya Mpunga katika bonde la Cheju Wilaya ya Kati Unguja ambalo mpunga wake umeharibika kwa kukosa mvua ambazo zilinyesha na kukata kuletea mpunga huu kuharibika na kuwakosesha mavuno wakulia wa bonde hilo lililo na heka karibu elfu kumi na saba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.