Habari za Punde

Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahaman Kinana Atembelea Ukumbi wa Mkutano Dodoma leo.

Jengo la CCM linalotarajiwa kufanyika kwa mkutano Maalum wa kumkabidhi Uwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli mwishoni mwa wiki hii Mjini Dodoma. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abduraham Kinana akisalimiana na Viongozi wa Jumuiya za CCM alipowasili katika jengo la Ukumbi wa Mkutano Mjini Dodoma kuangalia maandalizi yake kwa ajili ya Mkutano huo Maalum unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abduraham Kinana akisalimiana na Viongozi wa Jumuiya za CCM alipowasili katika jengo la Ukumbi wa Mkutano Mjini Dodoma kuangalia maandalizi yake kwa ajili ya Mkutano huo Maalum unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
Ukumbi wa Mkutano Maalum wa CCM ukiwa umekamilika kwa matayarisho yake kwa ajili ya Mkutano Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abduraham Kinana mwenye shati la kijani akimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Mhe. Nape Mnauye akitowa maelezo ya kukamilika kwa matayarisho ya ukumbi huo kwa ajili ya Mkutano Maalum unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii mjini dodoma. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abduraham Kinana akiwa katika Ukumbi wa Mkutano Maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii, alifika kuangalia matayarisho ya ukumbi huo. akiwa na Maofisa wa CCM.  
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Mhe. Nape Mnauye akimuonesha sehemu zilizoandaliwa kwa ajili ya washiriki wa mkutano huo Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahaman Kinana alipofika kutembelea ukumbi huo kujionea matayarisho yake yaliofanywa na Kamati ya Matayarisho ya Mkutano Maalum wa CCM. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahaman Kinana akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Mhe. Nape Mnauye wakati wa ziara yake kutembelea ukumbi huo leo mchana. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahaman Kinana akitembelea Ukumbi wa Mkutano Maalum wa CCM mjini Dodoma leo.Katibu Mkuun wa CCM Ndg Abdurahaman Kinana akizungumza na waandishi wa habari kukamilika kwa matayarisho ya Ukumbi wa Mkutano Maalum wa CCM, unaotarajiwa kufanyika wiki hii mjini Dodoma, na kusema wajumbe wote wa Mkutano huo watashiriki na wanatarajiwa kuaza kuwasili Mjini Dodoma kesho na wageni waalikwa kutoka Nje na Ndani kuthibitisha kushirika Mkutano huo wakiwemo Mabalozi walioko Tanzania wanaowakilishi Nchi zao Marais Wastaaf wa Tanzania na Zanzibar Makatibu Wakuu wa CCM Wastaf nao watashiriki katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.