Habari za Punde

Waziri wa biashara afanya uteuzi wa Wajumbe wa baraza la kusimamia mfumo wa utoaji leseni za biashara

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mh.  Amina Salum Ali kwa mujibu wa sheria ya kusimamia mfumo wa Utoaji Leseni za Biashara Nam. 13 ya mwaka 2013 amewateua maafisa 12 kuwa wajumbe  wa Baraza la kusimamia mfumo wa utoaji leseni za Biashara Zanzibar.

Uteuzi  wa wajumbe wa kusimamia mfumo wa utoaji leseni za Biashara  unafuatia uteuzi wa Mwenyekiti  wake uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhamed Shein.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko wajumbe walioteuliwa ni Hussein Migoda Mataka kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Ashura Mrisho Haji kutoka Wizara ya Habari, Utalii Utamaduni na Michezo na Amour Ali Mussa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za Serikali.

Wengine ni Hajar Idrisa Haji wa Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.  Abeida Rashid Abdalla wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu, Rashid Ali Salim Katibu Mtendaji Baraza la Kusimamia Mfumo wa Utoaji Leseni za Biashara na Omar Said Shaaban kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima (ZNCCIA)

Wajumbe wengine wa Baraza hilo ni Khamis Salum Ali kutoka ZNCCIA, Mohamed  Salim Mohamed wa Jumuiya ya Watembeza Watalii (ZATO), Salmin Sharif Khatib wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, Abdulaziz Hamid Mahmoud na Fatma Mussa Magimbi kutoka  sekta binafsi.

Uteuzi huo umeanza tarehe 24 August 2016.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.