Habari za Punde

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Azungumza na Walimu Wakuu wa Skuli za Mkoa wa Mjini Unguja

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma akizungumza na Walimu Wakuu wa Skuli za Mkoa wa Mjini Unguja za Serikali na Binafsi, katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Haile Seilasse, kujua changamoto zinazozikabili Skuli zao  ili kuweza kupatiwa ufumbuzi kuweza Wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao ya kila siku na kuongezeka kwa ufaulu. 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma akiwahutubia Walimu Wakuu wa Skuli za Mkoa wa Mjini katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Haile Salassie. Zanzibar.
Walimu Wakuu wa Skuli za Serikali na Binafsi wakimsikiliza Waziri wa Elimu Zanzibar Mhe Riziki Pembe wakati akizungumza na Walimu hao kujuwa changamoto zinazozikabili Skuli zao na njia ya kupzta ufumbuzi wake. 
Walimu Wakuu wakiwa ukumbi wa mkutano wakimsikiliza Waziri wa Elimu Zanzibar. 

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar akiwa na Uongozi wa Wizara ya Elimu wakisikiliza michango ya Walimu Wakuu wakati wa mkutano huo. uliofanyika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Haile Salasie Zanzibar.
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya High View Zanzibar Ndg. Ameir Hassan akichangia wakati wa mkutano huo wa kutowa changamoto zinazozikabili Skuli zao na mitaala ya Elimu kuwawezesha Wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao wakati wa mitihani ya Taifa.
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar Ndg. Ali Abdalla akichangia wakati wa mkutano huo wa Walimu Wakuu wa Skuli za Mkoa wa Mjini Unguja.
Mwalimu Mkuu Msaidi wa Skuli ya Msingi Kisiwandui Zanzibar Bi Kauthar akichangia mitaa la mitihani kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalumu utungwaji wa mitihani yao huo tafauti na kuwafanya kutofanya vizuri mitihani yao huja kama ya wanafunzi wa kawaida. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.