Mkuu wa Kitengo cha Lishe Wizara ya Afya Zanzibar Asha Hassan akizungumzia umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya mama pekee katika miezi sita ya mwanzo kama Lishe bora zaidi katika makuzi ya mtoto wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yaliyofanyika Mwera Wilaya ya Kati Unguja.
Afisa Lishe, UNICEF Dar es salaam Elizabeth Macha akitoa salamu za Shirika hilo katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya unyonyeshaji duniani yaliyofanyika kitaifa Mwera Wilaya ya Kati Mkoa Kusini Unguja.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohd Abdalla akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Mwera Wilaya ya Kati Unguja.
Naibu Waziri wa Afya Arusi Said Suleiman wa kwanza (kulia) akizungumza na akinamama waliohudhuria maadhimisho ya kilele cha wiki ya unyonyeshaji duniani katika kijiji cha Mwera Wilaya ya Kati Unguja.
Mmoja wa akinamama anaenyonyesha watoto wake maziwa pekee miezi sita ya mwanzo Raya Khamis akitoa ushuhuda na mafanikio anayopata kwenye kilele cha maadhimisho hayo.
NaRamadhani
Ali/Maelezo Zanzibar.
Shirika la Umoja wa
Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) limesisitiza umuhimu kwa Tanzania kuongeza
juhudi katika kuweka mikakati ya kuboresha unyonyeshaji wa watoto mara tu baada
ya kuzaliwa hadi kufikia miaka miwili.
Akitoa salamau za
kilele cha wiki ya unyonyeshaji duniani iliyoadhimishwa katika kijiji cha Mwera
Wilaya ya kati Unguja, Afisa Lishe kutoka UNICEF Dar es
Salam, Elizabeth Macha alisema utafiti wa 2014 unaonyesha ni mtoto
mmoja kati ya wawili wenye umri hadi kufiki miezi 23 wanaonyonyeshwa mara baada
ya kuzaliwa kwa Tanzania.
Alisema kwa Zanzibar
ni asilimia 61 tu ya watoto wenye umri kati ya miaka 0-23 wanaonyonyeshwa
katika muda wa nusu saa baada ya kuzaliwa na Mkoa wa Kusini Pemba upo nyuma
zaidi ukiwa na asilimia 52.
Aliongeza kusema kuwa
watoto wakicheleweshwa kunyonyeshwa kwa masaa 2 hadi 23 baada ya kuzaliwa
inaongeza hatari ya kufa katika siku 28 za kwanza za maisha ya mtoto kwa
asilimia 40.
Alisisitiza watoto
kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo bila kupewa
chakula chengine kwa vile yanamsaidia kukua vizuri kiakili na kimwili.
Alisema watoto
wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa Zanzibar ni asilimia 20 wakati Pemba
ina asilimia 10.
Afisa Lishe wa UNICEF
alisema kunyonyesha ni moja ya uwekezaji muhimu ambayo nchi inaweza kufanya kwa
ajili ya ustawi wa wananchi wake.
"Tunaweza kupata
maendeleo ya haraka katika maendeleo yetu endelevu kwa kukuza, kulinda na
kusaidia unyonyeshaji," alikumbusha afisa Lishe wa UNICEF.
Alisema iwapo mipango
mizuri ya kuboresha unyonyeshaji na kutekeleza kwa vitendo Tanzania inaweza
kufanya unyonyeshaji kuwa sehemu ya mwanzo katika kuimarisha afya kwa kila
mtoto na jamii kwa jumla.
Mkurugenzi wa Kinga na
Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohd Abdalla akimkaribisha mgeni rasmi
katika sherehe hizo alisema asilimia kubwa ya wanawake wananyonyesha watoto
lakini kasoro iliyopo ni kuwachelewa kuwanyonyesha, kuwalisha vyakula vyengine
wakiwa chini ya miezi sita na kuwaachisha maziwa kabla ya miaka miwili.
Naibu Waziri wa Afya
ambae alikuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji
duniani Arusi Said Suleiman aliwahimiza akinamama kuwanyonyesha watoto wao
maziwa pekee katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo kwani ni kinga bora kwa
afya zao.
Kauli mbiu ya
maadhimisho hayo "Unyonyeshaji ni kichocheo cha Maendeleo endelevu.
Dumisha unyonyeshaji kwa maslahi ya wote".
No comments:
Post a Comment