Habari za Punde

Bora Mwekezaji atoke Raia!


Na Mwandishi wetu
Asubuhi ya leo nimeamshwa na sauti ya mmoja ya walinzi anayelinda sehemu wakaazi wa Shangani tunoishi hapo tunapoegesha magari yetu. Niseme toka mwanzo kuwa sehemu hiyo imewekwa lami na mmoja wa wakaazi wa hapo ambaye ana hoteli hapo katika sehemu ya nyumba yao ya ukoo. 

Kwa maelezo ya mlinzi huyo kalazimika kuja kunigongea kwa sababu gari yangu imetishiwa kuvutwa na watu wa Manispaa kama haijaondoshwa. Nilipotaka kujua sababu za kuondosha gari nikaambiwa Mfalme anakuja Park Hyatt hawataki kuona magari. Nilimuuliza mlinzi huyo kama kuna taarifa rasmi zilokuja hapo ama na Manispaa au watu wa Park Hyatt kwani mimi sijapata barua au simu kunieleza lolote. Jibu ni kuwa mtu wao wa parking akiwaambia watu waondoe magari.

Nikataka kujua kuondoa gari kwa muda gani maana alipokuja Rais wa Ujerumani ilikua masaa kadhaa? Hakujakuwa na jibu. Nikauliza kama wameelekeza magari tukayaweke wapi kwa usalama? Tena sikupata jibu.

 Hakika taarifa nzima inaelekea kusambazwa kwa tetesi si kwa tamko au taarifa rasmi hivyo ni vigumu kujua amri imetoka wapi. Na wala hii si mara ya kwanza wakaazi kutakiwa kuondoa magari kwa sababu ya wageni wa Hyatt. Je hii ni haki? Ikumbukwe kuwa ujenzi wa Park Hyatt Mji Mkongwe ulizua tafrani kwa wakaazi wa mji mkongwe kwa namna eneo lilivyotolewa na hsusan kwa kukiuka sheria na taratibu za nchi.

 Hivyo kitendo cha kutaka wakaazi kuondoa gari zao ili kumpisha nwekezaji ni matokeo ya maamuzi yaliyofanyika yakipuuza maoni na maslahi ya wakaazi. Kwa mujibu wa sheria za Zanzibar kabla ujenzi au uwekezaji kufanyika ilibidi kwanza kufanyike tathmini ya mazingira yaani environmental assessment. Hapa palifanyika zoezi hilo maana suala kama egesho kwa ajili ya wageni wa hoteli ilibidi lizingatiwe. Tunaambiwa kuna egesho la chini kwa chini lilojengwa ndani ya hoteli ingawa hoteli zote sehemu ya Shangani wamehodhi sehemu za parking kiasi cha kwamba sasa pande zote mbili za barabara zinaegeshwa au magari yao au magari ya abiria yanayolenga biashara kwao.

Wakaazi wana muda mgumu kupata egesho au hata kutoka kutokana na msogamano. 

Kuna makala yamewahi kuandikwa kuhusu  athari ya kimazingira na kijamii yalosabbaishwa na ujenzi au uwekezaji wa Hyatt Shangani. 
Wakati kuna sheria kuhusu uzito wa gari zinazotakiwa kuingia Mji Mkongwe kwa siku kuna gari zinazopindukia  uzito huo zinazokuja kuleta maji hotelini. Itajengwaje hoteli kama hakuna maji ya kutosha? 

Leo kuna njia zimefungwa Mji Mkongwe eti kunusuru majumba kutokana na traffic ya magari wakati magari yanayoharibu majumba ni makubwa yanayokuja kuleta huduma kwenye mahoteli. 

Leo shangani mtaa mchafu umejaa taka za hoteli zilizopo. Ukitoa taarifa katika mamalaka husika hakuna hatua zinazochukuliwa maana hazitaki kukera wawekezaji. Shangani pamekua mtaa wenye kelele kutokana na mingurumo ya majenerata na ma A/c achilia mbali wafanya kazi wao.

Hizi hoteli zote zimeanzishwa katika makaazi ya watu wakiishi humo na wanaendelea kuishi. Serikali imewasaidia wawekezaji hawa kuchukua majumba yaliyokuwa chini ya uangalizi wao. Wameshi dwa kufanya hivi kwa majumba binfasi lakini hawashindwi kutoa amri na maagizo ambayo katika nchi yoyote inayoheshimu raia wake isingetjubutu seuze kuwaza kufanya. Leo katika nchi ya Kimapinduzi raia, tena mkaazi anaambiwa toka apishwe mfalme!

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.