Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza wakati wa majadiliano kuhusu upokonyaji wa silaha zikiwamo silaha za nyukilia. katika mchango wake Tanzania imezitaka nchi zenye silaha za nyukilia kuacha kutumia mabilioni ya fedha kujilimbikizia silaha za kijeshi na badala yake fedha hizo zitumike kusaidia maendeleo
Na Mwandishi Maalum, New York
Tanzania imeitaka
Jumuiya ya Kimataifa
kupunguza matumizi makubwa katika kujilimbikizia silaha zikiwamo za
maangamizi na badala yake fedha hizo
zielekezwe katika kusaidia utekelezaji
wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ( agenda 2030).
Wito huo umetolewa
siku ya jumanne na Mwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, wakati
Kamati ya Kwanza ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inayohusika
pamoja na mambo mengine, usalama wa kimataifa likiwamo
suala ya upokonyaji wa silaha
ilipokuwa ikijadilia ajenda ya
upokonyaji silaha.
“ Kila Septemba 26 ya kila mwaka, tunaadhimisha siku ya kimataifa ya kumaliza kabisa
silaha za nyukilia. Lakini wakati Kamati
hii ikianza mijadala yake hakuna hatua yoyote ya maana iliyochukuliwa ya kulimaliza tatizo hili” akasema Balozi Manongi
Na kuongeza, badala yake
dunia inashuhudia nchi ambazo
zinazomiliki silaha za nyukilia zikiendelea na kasi ya kuziongeza ikiwa ni pamoja na kuwekeza mabilioni ya dola katika kuzifanyia marekebisho na kuziimarisha.
“Kwa Tanzania, upokonyaiji
wa silaha na maendeleo ni mambo yanayohusiana. Kiasi cha
fedha ambacho kinaelekezwa katika matumizi ya
kijeshi yangeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa malengo
ya maendeleo endelevu. Ni kwa sababu hiyo tunaona umuhimu wa kazi za Kamati hii”.Amesisitiza Balozi.
Akizungumzia nafasi ya Umoja wa Mataifa katika kusimamia suala na upokonyaji wa silaha kupitia Taasisi zake, Balozi amesema licha ya ugumu na changamoto katika
eneo hilo. Tanzania bado inamatumaini
ya Umoja wa Mataifa kama
chombo muhimu kinachoweza kudhibiti
usambaaji wa silaha za maangamizi zikiwamo silaha ndogo ndogo, za kati na
nyepesi.
Pamoja na
kuelezea namna Nchi zenye silaha za maangamizi zinavyoendelea
kujilibikizia silaha hizo ikiwani
ni pamoja na kuziimarisha ili
ziwe za kisasa. Balozi pia ametumia
fursa hiyo kutahadharisha dhidi ya
hasara za kibinadamu zinazoweza kutokea dhidi ya matumzi ya silaha hizo.
Na kwa sababu hiyo,
Tanzania imezisihi nchi zinazomiliki
silaha za nyukilia kutumiza
wajibu wao kisheria ikiwa ni pamoja
na kuchukua hatua za kuangamiza silaha hizo kwa uwazi na bila kuchelewa na
kwa kuzingatia makubaliano ya
Mkataba wa Kimataifa wa
upokonyaji wa silaha.
Tanzania pia
imekumbushia haja na umuhimu wa nchi
ambazo hazina silaha za nyukilia kutonyimwa fursa ya kutumia teknolojia
ya nyukilia kwa shughuli salama
zikiwamo za utafiti na shughuli
nyingine za maendeleo na ustawi wa nchi
zao.
Kuhusu Ukanda Huru
zisizokuwa na silaha za nyukilia,
Tanzania ambayo ni nchi mwanachama wa Mkataba wa
Palendaba (Africa Nuclear Free
Zone) inaunga mkono uwepo wa Kanda huru
ambazo hazina silaha za nyukilia.
Katika hatua nyingine , Tanzania imekaribisha kuanzishwa kwa Benki ya
Teknolojia kwa nchi zilizonyuma
kimaendeleo ( Technology Bank for Least Developing Countries).
Kuanzishwa kwa bank hiyo
kunalenga pamoja na mambo mengine
kuzisaidia nchi za LDC’s kuwa na fursa
na uwezo wa kutumia teknolojia
sahihi kutoka kwa mataifa yaliyoendelea.
Hayo yameelezwa na Bw. Songalieli Shilla, Afisa Mkuu
Mambo ya Nje katika Uwakilishi wa
kudumu wa Tanzania wakati alipochangia kwa niaba ya Tanzania
majadiliano ya Kamati ya Pili ya Baraza
Kuu la Umoja wa Mataifa ilipokuwa ikijadili masuala mtambuka yakiwamo ya ukuaji
wa uchumi na maendeleo
Tanzania ikasisitiza kwamba kuanzishwa kwa Banki hiyo
kutazisaidia nchi za LDC’s kuingia katika ushindani na mataifa yalioendelea. Na kwamba
Tanzania inafarijika pia kwamba
Benki hiyo itaendelea kuzisaidia
hata zile nchi ambazo
zitakuwa zimefunzu kutoka nchi
zenye uchumi wa chini na kwenda kwenye uchumi wa kati.
Benki hiyo ambayo chimbuko lake ni mkutano uliofanyika mwaka 2011 nchini
Uturuki na ambayo tayari maandalizi ya awali yamekwisha kufanyika inatarajiwa kuzinduliwa
mwakani.
Kamati ya Pili ya
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inahusima na masuala ya Uchumi na Fedha,
na katika mkutano huo, pamoja na kukaribisha uanzishwaji wa Benki hiyo, pia
Tanzania imezungumzia changamoto mbalimbali ambazo zinakweza kukwamisha
utekelezaji wa ajenda ya maendeleo
endelevu hususani kwa nchi zinazoendelea.
Amazitaja baadhi ya
changamoto hizo kuwa ni pamoja na
mabadiliko ya tabia nchi,
upatikanaji wa raslimali fedha
kutoka vyanzo vya ndani na kutoka kwa wadau na washirika wa maendeleo.
Baada ya kukamilika kwa Mkutano na Majadiliano ya jumla ya
Baraza Kuu la 71 la Umoja wa
Mataifa, mkutano uliowakutanisha viongozi wakuu wa Nchi na
Serikali kutoka mataifa
mbalimbali duniani. Nchi wanachama wa
Umoja wa Mataifa, kupitia Kamati Sita zinazounda Baraza
Kuu la Umoja wa Mataifa, zimeingia katika ngwe nyingine muhimu ambapo
sasa wajumbe wanakutana
kupitia Kamati hizo kujadiliana
agenda na maazimio mbalimbali kuanzia yale yanayohusu uchumi, fedha na maendeleo, haki za binadamu, ustawi wa jamii, Amani na usalama,
umalizwaji wa ukoloni, utawala
wa sheria , sheria za kimataifa
na bajeti na utawala.
No comments:
Post a Comment