Habari za Punde

Makamo wa Rais wa Cuba Awasili Zanzibar kwa Ziara ya Siku Moja Apokelea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Uwanja wa Ngege wa Kimataifa wa Zanzibar.

Kikundi cha Ngoma cha Borafya kikitowa burudani ya Ngoma ya Kiluwa wakati wa Ujio wa Makamu wa Rais wa Nchi ya Cuba Nchini Zanzibar, kwa ziara ya Siku moja Zanzibar. 
Kikundi cha Sanaa cha Utamaduni Zanzibar wakicheza Ngoma ya Msewe wakati wa ujio wa Makamu wa Rais wa Cuba Salvadon Antonio.Zanzibar
Viongozi Serikali wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakisubiri kumpokea Makamu wa Rais wa Cuba Salvador Antonio.
Makamo wa Rais wa Cuba Salvador Antonio akipokelewa nma mwenyeji wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akiwa na shada la Au alilokabidhiwa baada ya kuwasili Zanzibar kwa ziara ya Siku moja Zanzibar.
Makamo wa Rais wa Cuba Salvador Antonio akiwa na mwenyeji wake Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipowasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Jiji Dar-es-Salaam 
Makamo wa Rais wa Cuba Salvador Antonio akikagua bwaride maalum aliloandaliwa wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuaza ziara yake ya Siku moja Zanzibar  
Makamo wa Rais wa Cuba Salvador Antonio akisalimiana na mwenyeji wake Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, baada ya kukagua bwaride rasmin aliloandaliwa wakati wa mapokezi yake alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuaza ziara yake ya siku moja Zanzibar.
Makamo wa Rais wa Cuba akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud alipowasili Zanzibar kwa ziara ya siku moja Zanzibar.
Makamo wa Rais wa Cuba akisalimiana na Meya wa Mji wa Zanzibar Mhe Khatib Abrahaman Khatib alipowasili Zanzibar kwa ziara ya siku moja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.