Habari za Punde

Mashindano ya wazi ya kuogelea yafanyika Zanzibar

 Washiriki wa mashindano ya wazi ya kuogelea Tanzania yaliyofanyika katika Bwawa la Skuli ya Kimataifa Zanzibar (Zanzibar International School) iliyopo Mazizini wakiwa tayari kuanza mashindano hayo.


 Muogeleaji Natalie Sanford Charlotte mwenye umri wa miaka tisa kutoka Morogoro International School alieshiriki michezo nane na kunyakuwa medali sita za dhahabu na mbili za fedha akiwaongoza wenzake na kuwa mshindi wa kwanza kwa upande wa watoto. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

 Mgeni rasmi wa mashindano ya wazi ya kuogelea Tanzania yaliyofanyika tarehe 8 na 9 mwezi huu, Khamis Abdalla ambae ni Katibu wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar akifuatilia mashindano hayo.

 Waogeleaji wa kigeni walioshiriki mashindano ya kuogelea ya wazi Tanzania yaliyofanyika Zanziba wakichuuano vikali katika mtindo wa back stroke huku wakiwaacha kwa mbali waogeleaji wazalendo.

 Muogeleaji bingwa wa mashindano ya wazi ya kuogelea Tanzania kwa upande wa watoto Natalie Sanford Charlotte akivishwa moja ya nishani ya dhahabu aliyonyakuwa katika mashindano hayo. Picha zote na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.