Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid na Viongozi wengine wakisubiri kumpokea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kulifungua Bunge hilo linalofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar. ikiwa ni mara ya Pili kufanyika Zanzibar mara ya kwanza limefanyika mwaka 2007 katika Ukumbi wa Baraza wa Zamani Kikwajuni Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Daniel .F. Kidega alipowasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani kwa ajili ya kulizindua Mkutano wa Bunge hilo mara hii linafanyika Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe, Zuberi Ali Maulid alipowasili katika viwanja vya Baraza Chukwani Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Afrika Mashariki Mhe Suzan Kolimba.
No comments:
Post a Comment