Habari za Punde

Wenye ulemavu washirikishwe katika katika masuala ya maendeleo - Wito

Na Salmin Juma

Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman ameishauri jamii inayoishi na watu wenye ulemavu kuwashirikisha katika masuala ya maendeleo na uchumi katika familia zao.

Amesema watu wenye ulemavu wana haki ya kushirikishwa katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo hivyo sio vyema kuwafungia ndani na kuwakosesha haki zao za msingi.

Ushauri huo umetolewa kwa niaba yake na katibu tawala wa mkoa huo, Yussuf Moh’d Ali wakati akikabidhi misaada ya mablanketi ya kuzuia mbu wa malaria yaliotolewa na shirika la shina INC yenye makao yake nchini Marekani ghafla ambayo ilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Kiislamu Ambasha wilaya ya Wete.

Amesema serikali inatambua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu na kupogeza juhudi zilizochukuliuwa na shirika hilo katka kuzipatia ufumbuzi changamoto  hizo.

“Naiomba jamii iwe na utaratibu wa kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika kupanga, kuchagua na kutekeleza shughuli za maendeleo katka familia zao na iache tabia ya kuafungia ndani kwani michango yao inahitajika”alishauri.

Mapema Rais wa shirika hilo, Jesca  Kamala  amesema shirika lake limekuwa likitoa misaada kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu ambao jamii inaonekana kuwatenga, kutowajali pamoja na kuyatelekeza.

Amefahamisha kuwa katika kujali kundi hilo shirika linaendelea na kazi ya kuwaendeleza kiuchumi watu wenye ulemavu  kwa kuunga mkono na kusaidia harakati za maendeleo wanazozianzisha.

Katika hatua nyengine Jesta ameikabidhi serekali ya mkoa mashine kumi na moja {11 } za kupimia presha na kuagiza zifikishwe katika Wizara ya Afya ili  zigawanywe katika vituo vya  afya kulingana na mahitaji.

Nae mratibu wa shina Pemba, Dadi Hamad Dadi, amesema mbali na kusaidiawatoto wanaoishi katika mazingira magumu pia shirika hilo linatowa ushauri wa kitaalamu katika kuwaendeleza wajasiriamali wa kilimo cha mboga mboga na upakasaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.