Habari za Punde

Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Wafanyamazungumzo na Waandishi wa Habari Zanzibar.

Na Ali Issa na Mwashungi Tahir / Maelezo Zanzibar.
MELI mpya ya Mapinduzi II inatarajiwa kuondoka nchini Jumaatatu ijayo kuelekea Mombasa chelezoni kwa kufanyiwa ukaguzi  wa kawaida  baada ya dhamana ya mwaka mmoja iliyowekwa kati ya Serikali na mtengenezaji wa meli hiyo.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mustafa Abuod Jumbe wakati akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisi ya Shirika la Meli Malindi Zanzibar
Amesema upelekaji wa meli katika chelezo ni suala la kawaida na halijaalishi kwa upya wa mwaka mmoja au miwili ispokuwa ni maamuzi ya Shirika kufanya hivyo.
Amesema wamepeleka chelezoni meli hiyo baada ya dhamana aliyotoa mtengenezaji ya mwaka mmoja kumalizika, hivyo ilipaswa kuchunguzwa kabla ya dhamana huyo kumalizika muda wake  Disemba mwaka huu.
Aidha amesema meli hiyo katika ukaguzi wake utakao fanywa nipamoja na kutia rangi ,ukaguzi wa viokozi ,mashine  ukungu na  mambo mengi yatayonekana kurekebishwa.
Amesema gharama ya matengenezo hayo yanatarajiwa kufikia dolazaidi ya 90 elfu ambapo zitagawiwa thuluthi tatu ,thuluthi moja mjenzi wa meli na sehemu mbili zilizo bakia zitatoa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hata hivyo aliwataka wananchi kuondosha hofu na wasiwasi kwa kuikosa meli hiyo  kwa kipindi kifupi na badala yake Shirika la Meli la Zanzibar limefanya mazungumzo na uongozi wa meli ya seling ili kuhudumuia usafiri kwa muda huo kwakwenda Pemba na Daresalaam mara tatu kwa wiki.
Pamoja na hayo Katibu huyo aliwambia wandishi wahabari kua Serikali ina mpango wa kununua meli mpya mbili ambayo moja itahudumia abiria pamoja na mizigo na nyengine itakuwa meli ya mafuta.   

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR


Picha no 1: Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliyano na Usafirishaji Zanzibari Mustafa Abuod Jumbe akizungumza na waandishi wa Habari  hawapo pichani huko Ofisi ya Shirika la Meli Malindi Mjini Zanzibar.
Picha no 2: Waandishi wa Habari wakichukuwa maelezo  ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji  Mustafa Aboud Jumbe wakati walipofika Ofisi ya Shirika la Meli Malindi Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.