Na Mwandishi Wetu.
Baada ya ligi ya msimu huu kuonekana kuanza na upinzani mkubwa na mashabiki wengi kuonekana viwanjani kutokana na hamasa iliyopo motisha umeanza kutolewa.
Katika kikao cha pamoja kati ya viongozi wa juu wa Sekreteriati ya ZFA, wakiongozwa na rais wa chama hico Ravia Idarous Faina na Kamati ya Ufundi leo hii kiliamua kutoa zawadi za kila mwezi kwa kuanza na upande wa ligi kuu.
Kwa kuanzia kamati hiyo ya Ufundi ya ZFA itaanza kutoa zawadi kwa mchezaji bora wa kila mwezi pamoja na mwamuzi bora wa mwezi.
Zoezi hilo litasimiwa na kamati hiyo kwa kushirikiana na ile ya waamuzi chini ya kamati tendaji ya ZFA.
Suala hili limeanza kupokelea kwa hisia nzuri na baadhi ya mashabiki walioanza kusikia taarifa hiyo na kuunga mkono jitihada hizo zinazoendelea kufanywa na ZFA tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi 2016-2017.

No comments:
Post a Comment