Habari za Punde

Balozi Seif amkagua Mhe Mapuri, afariji wafiwa wa aliyekuwa Mbunge wa Dimani


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimjulia hali Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar { ZEC } Mh. Omar Ramadhan Mapuri aliyelazwa Hospitali ya Rufaa Muhimbili Jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu kutokana na kudhoofika kwa afya yake.

Kati kati yao ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed akimpa pole Mh. Mapuri aliyelazwa Hospitali ya Muhimbili akipatiwa matibabu.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpa pole Bibi Shekha Mohammed Salum  Kizuka wa Mbunge wa Jimbo la Dimani Marehemu Hafidh Ali Tahir hapo matangani Kijijini kwa Mbunge huyo Maungani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Kulia ya Balozi Seif ni Kaka wa Marehemu Hafidh Ndugu Shibu Ali Tahir.

 Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Mama wa Marehemu Hafidh Ali Tahiri Bibi Mwanapili Juma Khamis wakati alipofika matangani kuipa pole Familia hiyo akitokea Jijini Dar es salaam Kikazi.

Kulia ya Bibi Mwanapili Juma ni Mkurugenzi wa Redio Bahari FM ambae ni mtu aliyefanya kazi kwa miaka mingi pamoja na Marehemu Hafidh Ndugu Yussuf Omar Chunda.

Picha na – OMR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.