Habari za Punde

Huduma ya maji yarudisha nyuma nguvu za akinamama


Na Salmin Juma, Pemba

Kufuatia msemo mashuhuri nchini  wa akina mama wakiwezeshwa wanaweza, imeonekana dhahiri kua wanaweza  kutokana na baadhi yao kuonekana wakijishuhulisha katika maeneo tofauti ya ukuzaji uchumi na maendeleo ikiwemo katika sekta ya kilimo, mifugo na hata uvuvi.

Hayo yamejidhirisha wazi jana katika ziara maalum ya waandishi wa habari kisiwani Pemba walipowatembeela wakulima wa mbogamboga ambao ni wanawake kutoka Mchangamdogo Wilaya ya  Wete mkoa wa kaskazini Pemba.

Akizungumza na waandishi wa habari hizi  Naibu mwenyekiti wa kikundi cha "TUNASONGMBELE"  wanaojishuhulisha na ukulima wa  Pilipili hoho, Tungule (nyanya) na Bilinganyi Bi Asha Khamis amesema kua, kutokana na hali halisi ya kimaisha ilivyokua ngumu kwa pamoja wameamua kujikusanya na kuunda kikundi kushikiriana katika sekata ya kilimo.

Amesema licha ya changamoto mbalimbali zinzowakabili ikiwamo soko la uhakika na kutokuwepo kwa huduma ya maji shambani mwao lakini mpaka hivi sasa nyota ya matumaini mema wameshaanza kuyaona.

 “kikundi chetu bado hakijakua na pia hatujaanza kugaiana faida, tunachokipata tunakiweka ili tuzidi kutanua mradi wetu kufikia malengo tuliyojipangia  na kwakweli tulichonacho tunashukuru” alisema Naibu huyo.

Akiitaja kwa mara nyengine tena  changamoto ya maji inayowakabili katika ushirika wao kwa hamasa amesema huwalazimu kuchukua huduma hiyo kutoka majumbani mwao na kumwagilia mazoa, hali ambayo inawatatiza na kuwapa usumbufu mkubwa.

Akijibu suala la mwandishi wa habari aliyetaka kujua uzalishaji wao ukoje pamoja na soko, amesema shamba lao ni la robo ekari na  tungule wanazozalisha kila msimu ni gari moja ya keri  hivyohivyo katika mazao mengine na soko bado ni tatizo  ambapo hutegemea  baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wanaojitokeza  kununua bidha hizo shambani kwao.

Bi Hadia Juma Hamad  mwanachama wa kawaida katika ushirika huo amesema kua, tokea kujiunga katika ushirika huo hali ya kiuchumi imekua afadhali ingawa bado hawajafika walipo pakusudia.

“lengo letu hasa na tukiwezeshwa kupatiwa huduma ya maji tulime eneo kubwa zaidi kwani eneo lipo ila maji tu ndio tatizo” alisema bi Hadia.

Ushirika wa "TUNASONGMBELE"  unajumla ya wanachama ishirini (20) kumi na nne katia yao (14) ni wanawake na sita (06) ni wanaume ambapo  wametoa wito kwa serikali  na taasisi binafsi kujitokeza kuwasaidia katika kutatua changamoto zao ili kufikia lengo walilolikusudia la kujikwamua kiuchumi na hatiame akinamama kupiga hatua za kimaendeleo zaidi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.