Habari za Punde

Katika kuadhimisha siku ya kisukari duniani, Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wafanyiwa vipimo

 Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wakifanyiwa vipimo vya afya na wafanyakazi wa Kitengo cha maradhi yasiyo ambukiza kwa kushirikiana na Wizara ya Afya.

 Meneja wa kitengo cha maradhi yasiyoambukiza Zanzibar Omar Mwalimu akimpa ushauri Bi. Asha Makame Ali, mfanyakazi wa Wizara ya Elimu, baada ya kufanyiwa vipimo na kubainika kuwa uzito wake hauendani na urefu alionao.
 Muuguzi kutoka kitengo cha maradhi yasiyoambukiza akimfanyia vipimo vya afya Mussa Hassan Zyuma wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali .

Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Muhammed Abdalla akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu ongezeko la maradhi ya kisukari na shindikizo la damu wakati wa kuwapima  wafanyakazi wa Wizara hiyo.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.